Home 2024 March 28 MYAHUDI NA MYUNANI HAWANA TOFAUTI…

MYAHUDI NA MYUNANI HAWANA TOFAUTI…

MYAHUDI NA MYUNANI HAWANA TOFAUTI…

Mara mbili, katika Kitabu cha Warumi; mara ya kwanza katika Warumi 3:22-23, na mara ya pili katika Warumi 10:12-13, Roho wa Mungu; kupitia andiko la Mtume Paulo, anatumia maneno, “Hakuna tofauti.”

Mara ya kwanza yametumika kuhusiano na hatia ya mwanadamu. Hapa, Wayahudi wa kidini, pamoja na watu wa Mataifa wasiomcha Mungu; watu wenye maadili ya kitamaduni, pamoja na washenzi walioshushwa hadhi, wote wanathibitishwa kuwa na hatia mbele za Mungu.

Katika sura tatu za kwanza za kitabu cha Warumi, mapendeleo yao na wajibu wao unazungumzwa kikamili, na hoja zao zimefikiriwa kwa uangalifu. Kisha inakuja hukumu yenye kutisha:

“HAKUNA TOFAUTI: KWA SABABU WOTE WAMEFANYA DHAMBI, NA KUPUNGUKIWA NA UTUKUFU WA MUNGU.”

Je! Si lazima kwamba, sisi sote tunapaswa kuinamisha vichwa vyetu chini kwa aibu na kukiri kwamba hati hiyo ya mashtaka ni ya kweli?

Je! Hatupaswi kukiri kwamba, hukumu yetu hiyo ni ya haki?

Kimsingi, kunaweza kukawa na tofauti kuhusu asili au kiwango cha dhambi zetu, lakini katika hili, bado hakuna tofauti: kwa kuwa sisi sote tumefanya dhambi; Na Mungu mwenye haki na mtakatifu, ni lazima alaani dhambi!

Hata hivyo, inaleta faraja, kuyapata tena maneno haya yakitumiwa tena mara ya pili kuhusiana na wokovu. Mara hii tena, Wayahudi wa kidini pamoja na Wasio Wayahudi wasiomcha Mungu wamejumuishwa, lakini wakati huu, tangazo hilo ni lenye neema na limejaa utukufu…

“KWA MAANA HAKUNA TOFAUTI YA MYAHUDI NA MYUNANI; MAANA YEYE YULE NI BWANA WA WOTE, MWENYE UTAJIRI KWA WOTE WAMWITAO; KWA KUWA, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA.”

Katika suala la dhambi, Mungu hawezi kuwa na ubaguzi. Hawezi kuwa mpole na tabaka fulani au vikundi ambavyo vinaonekana kuwa vimependelewa au vina faida kubwa zaidi. Wote wamefanya dhambi, na wote wanapaswa kuhukumiwa!

Mungu pia, wala haonyeshi upendeleo katika suala la wokovu. Mtu tajiri au mstarabu au mdini, wote hao hawapendelewi mbele ya wengine. Wasiojua kusoma na kuandika au wasio na maadili, wote ni wamoja; hawajatengwa. Sheria inawahukumu wote, lakini Kristo alikufa ili kuwaokoa wote, ili sisi sote “tuhesabiwe haki bure kwa neema yake.”

Rafiki, Je! Wewe umeokoka? Je! Uko sawa na Mungu?

KAMWE, huwezi kutumaini kukubaliwa naye, ikiwa unamwendea YEYE kwa sifa zako wewe mwenyewe binafsi, bali ikiwa tu unamwendea katika sifa za Yeye aliyebeba dhambi zako, huwezi kuachwa; “KWA MAANA YEYE YULE NI BWANA WA WOTE, MWENYE UTAJIRI KWA WOTE WAMWITAO; KWA KUWA, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA.”

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *