Home 2024 April 23 IMANI ‘YA’ YESU KRISTO

IMANI ‘YA’ YESU KRISTO

IMANI ‘YA’ YESU KRISTO

 “Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio …” (Warumi 3:22, SUV)

“Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio…” (Warumi 3:22, NEN)

Ni vyema ukitambua kuwa, Mtume Paulo katika mstari tajwa hapo juu, harejelei imani ‘KWA’ Yesu Kristo, bali anairejea imani ‘YA’ Yesu Kristo; Na wala harejelei kile ambacho Yesu Kristo aliamini, ila anarejelea kustahili kwake kuaminiwa, anarejelea usahihi wake, anarejelea uaminifu wake.

Hatupaswi kusahau kwamba imani ni jambo la ‘kubadilishana’; ni jambo la pande mbili. Upande mmoja ni huru (umejihakikishia); unaamini upande mwingine na upande mwingine ni binafsi (kipekee); ni tabia ya kuaminika. Upande mmoja unarejelea kile mtu anachofanya; upande mwingine kwa mtu jinsi alivyo. Kama mimi nina imani kwako, wewe unapaswa kuitunza imani hiyo pamoja nami; unapaswa kuwa mwaminifu.

Mara saba katika nyaraka zake, Mtakatifu Paulo anarejelea “imani ya Kristo” na katika mara zote hizo, kusudi lake limekuwa ni kusisitiza kustahili kwake Bwana wetu Yesu Kristo kupata uaminiko kamili kutoka kwetu. Kwamba, Mtakatifu Paulo, harejelei kuwa imani yetu kwa Kristo ndiyo huwa inaonekana dhahiri katika kila kisa. Katika kifungu tajwa hapo juu mtume huyo anatangaza kwamba haki ya Mungu, ambayo ni “kwa imani ya Kristo,” inatolewa “juu ya wote wanaoamini” – (Upande huu wa “wote waaminio” – ndiyo sehemu ya imani yako kwake).

Vile vile, katika Wagalatia 3:22 Mtakatifu Paulo anasema kwamba “andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.” Hapa tena, tunaamini kwa sababu Yeye anastahili tumaini letu.

Katika Wafilipi 3:9, Mtakatifu Paulo anaonyesha hamu yake ya kupata haki isiyokuwa yake mwenyewe, anasema “bali ile ipatikanayo kwa imani ya Kristo” – na kisha anaongeza: “haki itokayo kwa Mungu kwa imani.” Hapa kuna imani ya mwanadamu! Mwanadamu huyo ana imani katika Kristo kwa sababu Kristo ni mwaminifu (kabisa kabisa), anayestahili kuaminiwa (kabisa kabisa). Yeye alilipa, kwa ukamilifu, adhabu kamili kwa ajili ya dhambi zetu na sasa yuko mbinguni akitoa stahili za Kalvari – utajiri wa neema, rehema na masamaha ya dhambi.

Lakini kumbuka kwamba, “imani ya Kristo”, daima hutangulia (iko mbele ya) “imani yetu katika Kristo” – (imani yetu kwake). Je! Ingekuwa na faida (maana) gani kwetu, kumwamini Yeye (Bwana wetu – Yesu Kristo) kwa ajili ya wokovu wetu, kama hangetegemewa (hangeaminika) kabisa katika hili?

Naam, Yeye lakini; Anaweza kuaminiwa katika “kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye” (Waebrania 7:25). Hii ndiyo sababu Mtakatifu Paulo aliweza kumwambia yule mlinzi wa gereza aliyeogopa na kuwa na hofu nyingi kule Filipi kwamba:

“Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka” (Matendo 16:31)

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *