Home 2024 April 25 AHADI YA MUNGU vs JUHUDI ZA MWANADAMU!

AHADI YA MUNGU vs JUHUDI ZA MWANADAMU!

AHADI YA MUNGU vs JUHUDI ZA MWANADAMU!

“Maana ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika. Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa” (Warumi 4:14-15).

Hili linapaswa kujidhihirisha kwetu sote. Kama baraka ikipatikana kwa matendo ya Sheria, baraka hiyo ni malipo (umejitafutie kwa jasho lako); Ni mshahara wa kazi uliyoifanya. Hii ndiyo sababu Wagalatia 3:18 inasema: “Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Ibrahimu kwa njia ya ahadi.”

Mtume Paulo, mtume mkuu wa Mungu wa neema, anatangaza katika Warumi 4:4-5, kwamba:

“Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.”

Lakini ngoja turejee kwenye kifungu hiki cha maneno: “sheria ndiyo ifanyayo hasira.” Watu wengi kwa namna fulani hawalioni hili; Hawa, ni pamoja na baadhi ya ‘makasisi’ ambao wanatuambia kwamba Sheria ilitolewa ili kutusaidia kuwa watu wema. Lakini Mungu mwenyewe anasema kwamba, “sheria ndiyo ifanyayo hasira.” Kila mhalifu analijua hili, na kila mwenye dhambi anapaswa kulitambua hili pia; maana Mungu  kwa hakika, ameweka msisitizo mkubwa juu yake:

Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa…” (Wagalatia 3:19), “ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;” (Warumi 3:19). “kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (Warumi 3:20).

Kama tunamwendea Mungu huku tukitazamia uzima wa milele kwa sababu ya matendo yetu mema; Je! Si, kana kwamba sisi ndo tunamwekea Mungu masharti ya kutuokoa, ambayo kamwe Yeye hawezi kuyakubali?

Mungu, HAKIKA, hawezi kuuza wokovu kwa bei yoyote ile, achilia mbali kwa sababu ya matendo yetu machache “nzuri”, wakati sote ni mashahidi wa maisha yetu ambayo yamejawa kushindwa na dhambi…

Je! Tumaini letu pekee sasa ni nini? Mungu ameahidi kuwapa uzima wa milele wale wote wanaomtumaini Mwanawe (Yohana 3:35-36; Matendo 16:31; n.k).

“Karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *