Home Kuhusu Sisi

Kuhusu Sisi

SISI NI  NANI?
Grace Walk Ministry ni huduma ya bure ya Yesu Kristo inayoendeshwa na washiriki wa Mtembeo wa Neema kutokea Dar Es Salaam, hapa Tanzania.

“Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anaishi kwa vinywa vyetu, twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu”

– 2 Wakorinto 5:20

Madhumuni Yetu

Lengo letu ni kuhimiza huduma ya uaminifu kwa Mungu kupitia mafundisho ya Yesu Kristo sawasawa na Ufunuo wa ile SIRI.

“Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injli yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele”

– Warumi 16:25

Tunamhubiri Yesu Kristo, upatanisho kupitia damu yake, haki tuliyohesabiwa kutokana na ufufuko wake, maisha yenye ushindi yaliyofanywa ndani yetu kwa imani.

Tunafundisha Biblia haina makosa, tukiigawa kweli ya Neno la Mungu, tukiheshimu maagizo ya Mtume Paulo ya kuigwa kweli hiyo ya Neno la Mungu sawasawa.

Tunawafikia kwa huruma, watu wenye dhambi na waliokufa katika dhambi tukiwa na matumaini kwamba nao watakombolewa kama sisi, kwa neema ya Mungu, ili wawe na uzima wa milele.

“ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli” – 1 Timotheo 2:4

Fundisho Letu

Mafundisho yetu na Mahubiri yetu yanaanza na kukamilika katika Kristo Yesu, Bwana na Mwokozi wetu. Ikiwa ni kutoka kitabu cha Mwanzo mpaka Sheria ya Musa, kutoka Injili ya Ufalme mpaka ufunuo wa ile Siri, tunamhubiri Yesu Kristo pekee kuwa ndiye YOTE katika YOTE. Tunatambua kwamba Kristo alimteua na kumtuma Paulo kuwa Mtume wetu katika majira haya ya sasa. Hivyo ni katika maandishi ya Paulo pekee ndimo tunamopata fundisho, hadhi, mtembeo na hatima ya Kanisa – Mwili wa Kristo.

Kwao wenye masikio ya kusikia, tunawafundisha kwa ujasiri, kuanzishwa kwa Kanisa (Mwili wa Kristo) baada ya kuitwa Mtume Paulo (mid-Acts Pauline dispensation) huko tukiligawa Neno la Mungu kwa usahihi!

Tunachoamini

Katika kuenenda katika Neema ya Mungu iliyoachiliwa, huku tukiwa ni mabalozi wa ushirika wa Mungu


TUKIO LINALOFUATA

    There are no upcoming events at this time.


+
Twitter Followers
+
Facebook Likes
$
Total Donation
+
People Helped

RATIBA YA IBADA
Ibada ya Jumapili
Saa 3 asubuhi – Saa 8 Mchana

  • Sunday School
  • Kuimba na Kuabudu
  • Ibada
Ibada ya Jumanne
Saa 10:30 – Saa 12 Jioni

  • Mafundisho ya Biblia
Jumatano
Saa 10:30 – Saa 12 Jioni

  • Maombi ya watu wote kwa ajili ya kukulia wokovu
Alhamisi Saa
4 asubuhi – Saa 8 Mchana

  • Ushauri na Maombezi ya mtu mmoja mmoja 
  • Mazoezi ya sifa na kuabudu
Ijumaa: Saa
3 usiku – Saa 12 Asubuh

  • Mkesha
SHUHUDA

Nimetafuta kazi kwa miaka Mingi, nashukuru baada ya mchungaji kuniombea nipepata kazi-Amin.

Sanga Seta
Manager

Nimetafuta kazi kwa miaka Mingi, nashukuru baada ya mchungaji kuniombea nipepata kazi-Amin.

Lisa White
Choreographer

Nimetafuta kazi kwa miaka Mingi, nashukuru baada ya mchungaji kuniombea nipepata kazi-Amin.

Jaquline Emmanuel
Fashion Designer
VIDEO MPYA

VIONGOZI WA KANISA
Festus PattaAskofu
Hutuongoza katika ibada na kweli kumfuata Yesu wetu.
Linda MsakyMchungaji Kiongozi
Hutuongoza katika ibada na kweli kumfuata Yesu wetu.
Silivester GabrielMchungaji wa vijana
Hutuongoza katika ibada na kweli kumfuata Yesu wetu.
Beatrice FlorenceMchungaji Msaidizi
Hutuongoza katika ibada na kweli kumfuata Yesu wetu.

Comments are disabled.