Home 2024 April 07 DHAMBI INAUA KRISTO ANAOKOA!

DHAMBI INAUA KRISTO ANAOKOA!

DHAMBI INAUA KRISTO ANAOKOA!

Biblia Takatifu inasema wazi kwamba, “wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria” (Warumi 2:12).

Watu wengine hupuuza au husahau ukweli kwamba, mbali na Sheria, DHAMBI HUUA. Hili linadhihirika katika kila upande – Wivu, chuki, tabia mbaya na maisha machafu huharibu taswira njema ya mwanadamu na kuikengeusha.

Hii ndiyo sababu pia kwamba watu wengi katika nchi za ‘kipagani’ wanaishi kwa shida, nusu ya maisha yao yote; kwa sababu, “dhambi, ikiisha kukoma, huzaa mauti” (Yakobo 1:15) – mbali kabisa na sheria na hukumu!

Lakini Warumi 2:12 inaendelea kusema kwamba “wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria.” Hebu tafakari na hili pia…

Hapa, hebu angalia, mfano wa mtu ambaye anaanza kutumia madawa wa kulevya. Mtu huyu, kwa kadiri anavyozidi kuingia katika uraibu wa dawa hizo za kulevya, inambidi kuiba au kudanganya na kufanya utapeli ili aweze kupata pesa za kutosha kununua dawa hizo zaidi. Kwa kufanya hivyo, si kitambo kirefu, maisha yake yanaanza kuharibika; Na yeye anakuwa ni mtu aliyeanguka – mbali kabisa na sheria.

Lakini sasa, sheria inamkamata na hapa kunajitokeza jambo jipya kabisa; Anapelekwa mahakamani na kupatikana na hatia na kupelekwa jela. Hii ni adhabu ya kisheria kwa uhalifu wake, uhalifu ambao tayari ulikuwa ukimuangamiza, hata hivyo!

Kwa hiyo Sheria haiwafai (haiwasaidii) kitu wenye dhambi; ILA inaongeza tu hukumu ya haki ya dhambi kwa matokeo ya asili – na ya kusikitisha – ya dhambi.

Ndio maana, ni jambo lenye kupendeza sana, kujua kwamba kifo cha Kristo Yesu, pale Kalvari, ni suluhisho kamili kwa tatizo la wanadamu lenye sehemu mbili…

Warumi 5 inaeleza jinsi Kristo, hapo Kalvari, alivyokuja kutuokoa, katika hali zetu zote mbili: Kukosa nguvu ya kujiokoa na katika hukumu ambayo ilionyesha adhabu yetu.

Mstari 6: “Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.

Mstari 8: “…Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *