Home 2024 March 10 UHURU WA UTUKUFU WA WATOTO WA MUNGU

UHURU WA UTUKUFU WA WATOTO WA MUNGU

UHURU WA UTUKUFU WA WATOTO WA MUNGU

Sisi Watanzania, kwa zaidi ya miaka 60 sasa, tunasherehekea uhuru wetu kama taifa huru kuanzia hapo mnamo tarehe Tisa ya Disemba 1961.

Hata hivyo, haifuati tu moja kwa moja kutokana na ukweli huo kwamba, Watanzania wote sasa ‘wako huru’ – Mbali na hilo! Fikiria maelfu kwa maelfu ya walevi na waraibu wa dawa za kulevya, ambao wamefungwa kwa minyororo wanayotamani kuivunja. Wafikirie watumwa wa tamaa zisizo za adili, wa hasira kali, wasengenyaji wenye nia mbaya, achilia mbali wavuta sigara na wenye mazoea mengine mabaya ambayo hawawezi kuyadhibiti. Ndio kusema, idadi kubwa ya Watanzania ni watumwa wa-vizuri, na ukiyajumlisha yote katika neno moja, yanaitwa: DHAMBI!

Kama Mungu ni Hakimu mwadilifu – na NDIVYO ALIVYO, ni lazima aadhibu dhambi. Warumi 6:23 inasema: “mshahara wa dhambi ni mauti“, lakini kwa upande mwingine, Mungu na ashukuriwe, 1 Wakorintho 15:3 inasema: “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu“.

Bwana Yesu Kristo hakuwa mwenye dhambi; Hakuwa ametenda uhalifu wowote; hakukuwa na kosa alilolipia; Hakuwa na kifo cha kufa. Ilikuwa ni kifo chetu alichokufa pale Kalvari, na tunaokolewa kutokana na adhabu tunapotazama Kalvari na kusema: “Hiki si kifo chake anachokufa; ni kifo changu. Analipa kwa ajili ya dhambi yangu. Nitaikubali zawadi hii ya Mungu na kumwamini Yeye kama Mwokozi wangu”.

Huu ni ukweli wa kustaajabisha: Kifo, adhabu ya Sheria, ilitolewa juu yetu – katika Kristo. Kwa hiyo, Sheria (yaani, Amri Kumi), haina madai zaidi juu yetu; Kama ingekuwa hivyo, tungehukumiwa tena! Hii ndiyo sababu Mtume Paulo anasema katika Wagalatia 2:19: “Mimi kwa njia ya Sheria naliifia Sheria”. Sheria inaweza kumuua mtu, lakini baada ya hapo, Sheria inaweza kufanya nini tena cha zaidi? Haiwezi kufanya kitu chochote tena! Sheria imemuua, huyo mtu, (katika Kristo) na kumweka huru kutoka katika utawala wake yenyewe!

Ewe rafiki ambaye hajaokoka bado, Mungu anataka uwe huru; Uwe huru kwelikweli. Yeye mwenyewe, alilipa adhabu ya dhambi kwa ajili yako na anataka ufurahie kile Mtume Paulo anachokiita, “uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu” (Warumi 8:21), uhuru kutoka kwenye hukumu ya Sheria!

Weka imani yako kwa Kristo Yesu ambaye alikufa kifo chako na utapata kuona jinsi kweli ya utukufu ilivyo kwamba, “Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli” (Yohana 8:36).

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *