Home 2023 March 04 REJEO LA MSALABA!

REJEO LA MSALABA!

REJEO LA MSALABA!

Kama kuna jambo ambalo Biblia inaliweka wazi zaidi kuliko jambo lingine lolote lile, ni kuhusu ukweli kwamba siri ya habari njema zote za Mungu kwa mwanadamu zimejikita pale Kalvari. Ilikuwa ni kwa sababu Kristo alipaswa kufa kwa ajili ya dhambi ndipo Mungu angeweza kutangaza habari njema kwa wenye dhambi katika vizazi vyote.

Ilikuwa ni hadi muda fulani kupita baada ya kusulubishwa Kwake, ndipo “kuhubiriwa kwa msalaba” kulitangazwa sana kama ujumbe na Mtume Paulo katika “injili [habari njema] ya neema ya Mungu” (Matendo 20:24; 1 Wakorintho 1:18).

“Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.”

“Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.”

Tangazo la “injili ya neema ya Mungu” lilikuwa ni usindikizaji wa asili kwa ufunuo wa msalaba kama siri ya habari njema ya Mungu kwa mwanadamu. Katika tangazo hili la neema yake iliyo nyingi (tele) kwa wenye dhambi, kila kitu kimejikita katika msalaba.

Kulingana na nyaraka za Mtume Paulo “tuna ukombozi wetu kupitia damu yake [Kristo]” (Waefeso 1:7), “tumehesabiwa haki kwa damu yake” (Warumi 5:9), “tumepatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake.” (Warumi 5:10), “tumefanywa kuwa karibu kwa damu ya Kristo” (Waefeso 2:13) na “tumefanywa kuwa haki ya Mungu katika Yeye” kwa sababu Mungu “alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu” (2 Wakorintho 5:21).

“Agano” la sheria lilifutwa na msalaba (Wakolosai 2:14), laana ya torati (sheria) iliondolewa na msalaba (Wagalatia 3:13), “kiambaza cha kati kilichotutenga” kilivunjwa (kilibomolewa) na msalaba (Waefeso 2:14) na wanaomwamini Kristo “wamepatanishwa na Mungu katika mwili mmoja” kwa msalaba (Waefeso 2:16). Si ajabu kwamba Mtume Paulo anaita ujumbe wake “kuhubiriwa kwa msalaba”!

Kwa mwamini mwaminifu, inasisimua kuona msalaba kama jibu la Mungu kwa Shetani wakati, kwa mtazamo wa kwanza, ilionekana kwamba Kalvari ilikuwa ushindi mkuu zaidi wa Shetani!

Hivyo, hima sote, tuseme pamoja na Mtume Paulo kwamba:

“Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo!” (Wagalatia 6:14)

UTUKUFU UNA YEYE KRISTO MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

5 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *