Home 2021 April 14 Neno Moja Tu!

Neno Moja Tu!

Neno Moja Tu!

Akizungumzia Hekalu kubwa la Mungu, ambalo Mfalme Daudi alitarajia sana kulijenga, alisema:

“Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake” (Zaburi 27:4)

Vivyo hivyo, Martha wa Bethania alipomlalamikia Yesu kwamba Mariamu “aliketi miguuni pake na kusikia Neno Lake” wakati yeye alikuwa akiachwa ahudumu peke yake, Bwana alijibu:

“Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa” (Luka 10:41-42)

Leo, kwa habari ya ujumbe wa neema kutoka kwa Bwana wetu aliyepaa juu, na aliyetukuzwa, Mtume Paulo anatuhimiza: “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu…” (Wakolosai 3:16). Matokeo ya kupendeza huwa yanafuatia baada ya azimio kama hilo la kumjua Kristo kupitia Neno.

Wakati ule Bwana Yesu alipomfungua macho mwombaji kipofu, ndugu huyo maskini alishambuliwa vikali, punde baadaye, na viongozi wa dini wa wakati huo. Yeye, hata hivyo, hakuweza kuwajibu maswali yao yote lakini aliweza kujibu jambo moja tu muhimu zaidi kwake:

“Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nalikuwa kipofu na sasa naona” (Yohana 9:25)

Simulizi iliyobakia inaelezea jinsi yule ombaomba kipofu pia alivyopata ‘kuona kiroho’, baada ya kuonana tena uso kwa uso na Mwana wa Mungu: “Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia” (Mstari wa 38).

Lakini je, ni upi mwenendo wetu baada ya kupata ‘uona wa kiroho’? Muumini ‘aliyepakwa mafuta’ zaidi atakiri kwamba mara nyingi anashindwa kuishi kulingana na ‘nuru aliyopokea’. Mtume Paulo, anatupa suluhisho la tatizo hili, pale aliposema:

“Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu” (Wafilipi 3:13-14)

Kwa utukufu wa JINA, lipitalo majina yote!

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *