Home 2024 March 03 KUSHINDWA MARA SABA!

KUSHINDWA MARA SABA!

KUSHINDWA MARA SABA!

Pamoja na mwelekeo wa asili wa mwanadamu wa kujisifu, historia imethibitisha tena na tena kwamba yeye ni mtu asiyefaa, na anayemhitaji sana Mungu na neema Yake. Ikumbukwe kwamba:

Enzi ya kutokuwa na hatia ilifungwa kwa mwanadamu kumwasi Muumba wake na kuwa kiumbe aliyeanguka, mwenye dhambi (Warumi 5:12).

Enzi ya Dhamiri ilifunguliwa kwa kesi ya mauaji (Mwanzo 4:8) na kabla ya enzi nyingine kuingizwa “dunia ilijaa dhuluma” (Mwanzo 6:11).

Kisha ikaja enzi ya Serikali ya Kibinadamu, lakini mtawala wa kwanza wa ulimwengu alijifanya kuwa ‘tamasha’, akakaa uchi, kwa sababu ya ulevi (Mwanzo 9:20-21). Si ajabu kuona kwamba, punde kidogo, tunaiona jamii ‘iliyolewa’ na ‘mambo yake yenyewe” na ilimbidi Mungu avuruge lugha yao pale Babeli (Mwanzo 11:4, 7-8).

Enzi ya Ahadi ilifuata, huku Ibrahimu akishindwa kuingia katika nchi ya ahadi kwa sababu ya kutokuamini (Mwanzo 15:7-15, 17:17). Enzi hiyo, ilifungwa na Israeli, uzao wake, kushindwa kuingia katika nchi ya ahadi kwa sababu ya kutokuamini pia (Waebrania 3:19).

Enzi ya Sheria ilianza kwa Israeli kuabudu ndama wa dhahabu kabla hata Musa hajashuka kutoka Sinai (Kutoka 32:1). Si ajabu, enzi hiyo, iliisha kwa Israeli kumkataa Kristo!

Enzi ya Neema ilianza na kuitwa kwa Mtume Paulo, balozi wa Mungu wa upendo na neema, ambaye aliteswa na kufungwa (Waefeso 6:20). Hii ilionyesha mtazamo wa mwanadamu juu ya Mungu na neema Yake. Enzi hiyo nayo italetwa mwisho (itafungwa), kwa kadiri mwanadamu anavyokomaza shingo yake katika kuendelea kwake kutenda dhambi badala ya kuikubali neema ya ukombozi wa Mungu katika Kristo (2 Wakorintho 4:4; 2 Timotheo 3:1-5).

Enzi ya ufalme wa Kristo, ambayo itafuatia enzi hii ya sasa ya Neema ya Mungu, itaanza kwa Bwana wetu kuyakemea mataifa yenye nguvu (Mika 4:3) na itafungwa kwa umati wa watu, ambao kwa muda, watakuwa wametoa ridhaa (watakuwa watii) kwa kulazimishwa, wakimfuata Shetani (Ufunuo 20:7-9).

Haya yote, yanaonyesha jinsi mwanadamu anavyomhitaji Mungu na wokovu wake kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo!

“Wote wamefanya dhambi” (Warumi 3:23) lakini, ashukuriwe Mungu kwamba: “Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka” (Warumi 10:13).

Pamoja na ukweli kwamba, mwanadamu amezungukwa na dhambi na uasi, watu wengi katika historia, wameliita JINA LA BWANA na wameokolewa!!!

Wewe je, UNANGOJA NINI???

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *