Home 2024 February 17 Jinsi Mungu Anavyowatia Nguvu Mashahidi Wake

Jinsi Mungu Anavyowatia Nguvu Mashahidi Wake

Jinsi Mungu Anavyowatia Nguvu Mashahidi Wake

Kama tujuavyo, Mtume Paulo alifanya miujiza mikubwa, kama Mtume Petro na waumini wa Kipentekoste walivyofanya, baada ya udhihirisho wa ile siku ya Pentekoste. Kimsingi, ulinganisho wa miujiza ya Mtume Paulo na ile ya Mtume Petro unaonyesha kuwa miujiza ya Mtume Paulo ilikuwa na nguvu zaidi kuliko ile ya Mtume Petro:

“Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida” (Matendo 19:11)

Hii hasa, ilikuwa ni katika uthibitisho wa kimungu wa utume wake, kwa kuwa Mtume Paulo hakuwa mmoja wa wale mitume kumi na wawili wa Yesu, katika mwili (2 Wakorintho 12:11-12).

Lakini ni jambo lililo wazi, kutokana na mapitio ya huduma ya Mtume Paulo na nyaraka zake, kwamba madhihirisho haya ya kimiujiza yangetoweka kadiri kipindi cha neema kilipoingizwa kikamilifu (angalia 1 Wakorintho 13:8; Warumi 8:22-23; 2 Wakorintho 4:16 – 5:4; 12:10; Matendo 28:7-9; Wafilipi 2:27; 3:20-21; 1 Timotheo 5:23; 2 Timotheo 4:20). Kwa hakika, katika nyaraka zote saba (7) za mwisho za Mtume Paulo (yaani, baada ya Matendo 28); hakuna chochote kinachosemwa kuhusu ishara, miujiza, uponyaji, lugha, maono wala kutoa pepo…!!!

Basi Je! Mungu anawatiaje nguvu watumishi Wake katika mapambano yao na Shetani na mapepo yake? Jibu ni kwa Roho Mtakatifu kupitia Neno Lake, linapohubiriwa kwa usadikisho. Kuna kiasi kikubwa cha ushahidi kuhusu hili katika nyaraka zote za Paulo, ikiwa ni pamoja na zile nyaraka zake saba (7) za awali. Angalia hii mifano miwili:

  • 1 Wakorintho 2:4:

“Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu.”

Angalia vyema hapo, kwamba hii ilikuwa ni nguvu katika mahubiri yake, na sio nguvu katika kufanya miujiza. Ni hakika kwamba, wakati ule ule ambapo Mtume Paulo alipoutangaza ujumbe wake aliopewa na Mungu kwa uwezo huo, yeye mwenyewe alikuwa ni mdhaifu sana, kwani katika Aya iliyotangulia amesema maneno haya, kuwa: “Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi.

  • 1 Wathesalonike 1:5:

“Kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.”

Huko Thesalonike, Mtume Paulo pia alikuwa amepatwa na upinzani mwingi na mateso, hadi mji mzima ukawa katika ghasia kuu (Matendo 17:1-5), na hii inaweza kuwa pia ni matokeo ya mahubiri yake hayo yenye nguvu. Hata hivyo, kutoka kwenye “msukosuko” huo, kulizaliwa (kulizuka) kanisa pendwa la Thesalonike, kielelezo na msukumo kwa wale walioletwa kwa Kristo wakiwa katika hali mbaya zaidi ya hiyo.

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *