Home 2023 April 10 Mantiki ya Mpango wa Wokovu

Mantiki ya Mpango wa Wokovu

Mantiki ya Mpango wa Wokovu

Katika1 Wakorintho 1:22 tunaambiwa kwamba “Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima.” Bila shaka hii ndiyo sababu Mungu alimchagua Mtume Paulo, pamoja na historia yake ya kina ya kiakili na ufahamu, kumtangaza “Kristo aliyesulubiwa,” ni “nguvu ya Mungu” na “hekima ya Mungu” (1 Wakorintho 1:23,24).

Mtume Paulo alikuwa mwana mantiki mwenye kipawa pamoja na mwanatheolojia mbobevu, na hakuna mahali ambapo jambo hili linadhihirika zaidi kama katika waraka wake kwa Warumi, ambapo, kwa uvuvio wa kimungu, anawasilisha mantiki ya mpango wa Mungu wa wokovu. Tena na tena, katika waraka huo wote, anatumia neno lile lile lililo maarufu sana katika hisabati na katika mantiki: “kwa hiyo.”

  • Kwa hiyo, … huna udhuru…” (Warumi 2:1)
  • Kwa hiyo hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria” (Warumi 3:20)
  • “Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria…. Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani, pasipo matendo ya sheria” (Warumi 3:21,28)
  • Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, tuna amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye kwa yeye tunaweza kupata…” (Warumi 5:1-2)
  • “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 8:1)
  • Basi, ndugu, tuna deni…” (Warumi 8:12)
  • Basi nawasihi…itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana (Warumi 12:1)

Ni sheria isiyoweza kugeuzwa, isiyobadilika kwamba dhambi hutokeza kifo. Lakini Bwana Yesu Kristo, “ambaye hakutenda dhambi,” alichukua mahali petu na “alikufa kwa ajili ya dhambi zetu.” Hivyo pia ni sheria isiyobadilika kwamba “Yeye aliye naye Mwana anao uzima.” “Sheria ya Roho” ni “uzima katika Kristo.” Wakati mtu anapomwamini Kristo Yesu kama Mwokozi wake, Roho Mtakatifu humpa uzima; uzima wa Kristo, ambao ni wa milele – hakika, ni uzima wa milele (Warumi 8:2; 1 Yohana 5:12).

UTUKUFU UNA YEYE MUNGU MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *