Home 2023 January 10 MAAGIZO YA BWANA

MAAGIZO YA BWANA

MAAGIZO YA BWANA

“Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.” (1 Wakorintho 14:37).

Wakristo wengi wana mawazo yaliyochanganyikana na wanadhani kwamba Kristo alipopaa kutoka Mlima wa Mizeituni kwenda mbinguni, aliacha kusema. Lakini hakuna kitu kinachoweza kuzidi na kuwa zaidi ya ukweli!

Mtume Paulo anasema kwamba mambo aliyowaandikia Wakorintho, na kwa Mwili wa Kristo kwa ujumla, yalikuwa ni “maagizo ya Bwana”! Vivyo hivyo, katika waraka wake kwa Wathesalonike, Mtume Paulo anasema, “Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu” (1 Wathesalonike 4:2).

Baada ya Kristo Yesu kupaa mbinguni, taifa la Israeli liliendelea katika uasi wake dhidi ya Mungu kwa kukataa huduma ya Roho Mtakatifu kupitia wale Thenashara kumi na wawili. Kwa hiyo, Israeli iliwekwa kando kwa muda na Mungu (Matendo 7). Kisha Mungu akamwinua mtume mpya, na kumpa ujumbe ambao haujawahi kufunuliwa kwa mtu yeyote kabla yake (Matendo 9; Wagalatia 1:11-12). KRISTO ALISEMA TENA!

Kutoka mbinguni Kristo aliyetukuzwa alimpa Mtume Paulo ufunuo mpya kuhusu huduma yake ya mbinguni kwa Kanisa, Mwili wa Kristo. Kwa Mtume Paulo pekee, mtume wa Mataifa (Warumi 11:13), zilitolewa amri za Kristo kwa ajili ya Mwili wa Kristo leo. Katika nyaraka za Mtume Paulo, ndimo tuyaonamo mapenzi ya Mungu kwa maisha yetu ya Kikristo wakati wa kipindi hiki cha neema ya Mungu. Katika nyaraka za Mtume Paulo, ndimo pekee tunapata mafundisho ya neema ambayo Kanisa limejengwa juu yake na linapaswa kuishi kwayo na kuyashirikisha kwa ulimwengu.

Tambua kwamba maneno ya Mtume Paulo, kama yalivyofunuliwa Kwake na Kristo, yamesemwa kuwa ni “MAAGIZO.” Hili si neno la kujichagulia kulichukua-au-kuliacha. Agizo linapotolewa na Mungu, Yeye hututarajia sisi kulitii ili kuyapatanisha mapenzi yetu na mapenzi yake. Katika nyakati zilizopita, amri nyingine zilitolewa ambazo zilikuwa halali kwa wakati ule zilipotolewa, lakini si za leo, na si kwa ajili ya utendaji wetu leo.

Angalia mfano wa chakula. Biblia inamuamuru mwanadamu kula mboga na matunda tu pale mwanzo, kisha ikamruhusu kula nyama, matunda na mboga mboga, baadae kidogo ikaamuru vyakula fulani tu kuliwa, mwishowe ikaamuru kwamba vyakula vyote vinaweza kuliwa. Haiwezekani kutii amri hizi zote tofauti kwa wakati mmoja…!

Kuna maswala mengine mengi katika Maandiko yanayolingana na haya, kwa hivyo ni muhimu kuamua ni maagizo gani ambayo Mungu anayataka sisi tuyatii leo. Jibu ni kwamba nyaraka za Mtume Paulo ni amri za Bwana ambazo ni halali kwa nyakati hizi za leo chini ya neema. Ni vyema sana kuishi chini ya NEEMA; nyakati ambayo Mungu yumo!

UTUKUFU NA UWEZA UNA YEYE MILELE NA MILELE. AMINA.

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *