Home 2022 November 13 Paulo, Mjenzi Mkuu!

Paulo, Mjenzi Mkuu!

Paulo, Mjenzi Mkuu!

Katika 1 Wakorintho 3:10, Mtume Paulo anatangaza kwa maongozi ya Roho Mtakatifu kwamba:

“Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.”

Je! Ni katika maana gani, Mtume Paulo alikuwa ni mjenzi mkuu wa Kanisa, na ni “msingi” gani aliuweka?

Je! Yeye mwenyewe hakusema kwamba “msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo”? (1 Wakorintho 3:11)

Ndiyo, alifanya hivyo – na ni katika kifungu hiki hiki!

Hakutafuta kuweka msingi mwingine isipokuwa Kristo, lakini Mungu alikuwa amemchagua yeye kumtangaza Kristo kwa namna (njia) mpya.

Miaka kadhaa iliyopita, Bwana wetu Yesu Kristo, alikuwa amewauliza wanafunzi Wake hivi: “Ninyi mwaninena mimi kuwa ni nani?” (Mathayo 16:15); Simoni Petro, mara moja, alimjibu akisema: “Wewe ndiwe Kristo [Masihi], Mwana wa Mungu aliye hai” (Mathayo 16:16). Hivi ndivyo waumini kwa ujumla walivyokuwa wakimtambua wakati huo (Yohana 1:49; 6:69; 11:27; 20:31). Kwa hakika, ufalme wa Kimasihi ungejengwa juu ya Kristo akiwa Mwana mpakwa-mafuta wa Mungu (Masihi humaanisha “mpakwa-mafuta”).

Lakini kwa kuinuliwa kwake Mtume Paulo, Mungu alianza kufanyiza “Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo” (Waefeso 1:22-23; Wakolosai 1:24-25). Hili ndilo Kanisa la leo, na limejengwa, si juu ya Kristo kama Mfalme, bali kama Bwana aliyeinuliwa (aliyetukuzwa) na ambaye ni Kichwa cha “mwili mmoja” (1 Wakorintho 12:13).

Mtume Paulo hamwasilishi Kristo kama Masihi, bali humwasilisha Kristo kama Bwana. Katika Warumi 10:9 anatangaza hivi:

“Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”

Tena katika 1 Wakorintho 12:3 Mtume Paulo anatangaza hivi:

“Hakuna mtu awezaye kusema kwamba Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”.

Na tena katika Wafilipi 2:9-11, Mtume Paulo anatangaza haya:

“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”

Je; Wewe umemkiri YESU KRISTO kuwa BWANA???

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *