Home 2021 November 09 Matendo Mema

Matendo Mema

Matendo Mema

Mamilioni ya watu leo wanajitahidi wenyewe ‘kujifanya’ wakubaliwe na Mungu kwa kutenda matendo mema. Watu kama hao hawawezi kamwe kuwa na uhakika wa wokovu wao, kwa sababu rahisi tu kwamba hawawezi kamwe kuwa na uhakika kama kweli wamefanya kazi njema ya kutosha na/au kama wamezifanya kwa njia ifaayo. Wengine wanadhani kwamba mbingu zinaweza ‘kutekwa’ kama matendo yao mema yanazidi matendo yao maovu; lakini hilo pia halina maana, kwa sababu matendo mema ndiyo ambayo sisi sote tunapaswa kuyafanya na kwamba hata tendo moja ovu linaweza kumzuia Mungu mwenye haki na mtakatifu asituhesabie haki na/au asituingize katika uwepo wake.

Hebu tusiweke ‘mkokoteni’ mbele ya punda! Mungu anatarajia matendo mema kutoka kwa watoto wake lakini si kama malipo ya wokovu wao, kwa kuwa uzima wa milele na utukufu haviwezi kununuliwa kwa bei yoyote ile. “Kristo Yesu alikuja ulimwenguni,” asema Mtume Paulo, “kuwaokoa wenye dhambi” (1 Timotheo 1:15). Kisha, akiwa amekwisha kuwaokoa kwa neema, anawatazamia wafanye matendo mema kwa shukrani.

Ni vyema hapo tukilinganisha Tito 3:5 pamoja na Tito 3:8:

Tito 3:5: “Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi, bali KWA REHEMA YAKE ALITUOKOA.”

Tito 3:8: “…mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, ILI WALE WALIOMWAMINI MUNGU WAKUMBUKE KUDUMU KATIKA MATENDO MEMA…”

Imani ni mzizi; matendo mema ni matunda. Hivyo tunasoma katika Waefeso 2:8-10 maneno haya ya Mtume Paulo:

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu; ni kipawa cha Mungu; WALA SI KWA MATENDO, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, TUTENDE MATENDO MEMA, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”

Kwa Utukufu Wake Kristo Yesu

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *