Home 2021 October 13 JAMBO MOJA MUHIMU!

JAMBO MOJA MUHIMU!

JAMBO MOJA MUHIMU!

Umuhimu wa Neno la Mungu katika maisha ya Mkristo umewekwa wazi, mara moja na kwa watu wote, katika moja ya kumbukumbu iliyovuviwa ya moja ya ziara za Bwana wetu Yesu Kristo nyumbani kwa Mariamu na Martha:

“Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa” (Luka 10:38-42)

Maoni juu ya kifungu hiki kwa ujumla yanaonyesha kuwa Mariamu na Martha, wote wawili, walikuwa na ‘sehemu’ yao nzuri! Hili, huenda likawa ni kweli, lakini kama tunajizuia sisi wenyewe kuwa na maoni zaidi ya hayo, tutakuwa hatujalitendea haki kusudi la umilele lililokusudiwa na Mungu katika  fundisho lake hilo, kwani hata Bwana wetu mwenyewe hakuwapongeza akina dada hao wote wawili kwa sababu ya “sehemu yao hiyo nzuri”. Bwana Yesu, kimsingi, alimkemea Martha na akampongeza na kumtetea Mariamu kwa jambo moja la msingi.

Je! Mariamu hasa alipongezwa kwa nini? Je! Ni mara ngapi ameonyeshwa kama mfano bora kwetu katika kuutumia muda wetu mwingi na Bwana katika maombi? Hata hivyo, huko ni kukosa maana sahihi ya kifungu hiki. Mariamu hakuwa akiomba; Bali “aliketi miguuni pa Yesu, akisikia NENO LAKE.” Alikaa tu pale, ‘akinywa’ kila kitu alichosema Yesu. Hili lilikuwa “jambo moja muhimu” ambalo Mariamu alikuwa “amelichagua” na ambalo Bwana wetu alisema halingechukuliwa kutoka kwake.

Kwa hivyo, wakati sala na ushuhuda na kazi njema zote zina umuhimu katika maisha ya mwamini, kusikia Neno la Mungu ni “jambo moja muhimu zaidi” juu ya mengine yote. Hakika, tuache hiki “kitu kimoja” kipewe nafasi yake stahiki na yote mengine yatafuata kikawaida.

Ni jambo lililowazi kwamba ni lazima tujifunze Neno la Mungu kwa maombi na kwa moyo ulio wazi, la sivyo linaweza kuwa na madhara kwetu badala ya kuleta matokeo yenye faida. Lakini, hata hivyo, hili linaendelea kutuwekea mkazo zaidi juu ya umuhimu mkubwa wa Neno la Mungu, ambalo tunalitafuta, kwa kusoma kwa dhati na kwa maombi, ili tulielewe na kulitii.

Kwa Utukufu Wake Kristo Yesu

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *