Home 2021 July 11 Kumgawa Roho Mtakatifu Sawasawa

Kumgawa Roho Mtakatifu Sawasawa

Kumgawa Roho Mtakatifu Sawasawa

Tutakuwa hatujafanywa makosa tukiigawa huduma ya Mtume Petro na huduma ya Mtume Paulo. Mtume Petro na Mtume Paulo, wote wawili walimhubiri Yesu Kristo, lakini kwa njia tofauti.

Mmoja alimhubiri Kristo kulingana na ‘unabii’, na mwingine alimhubiri Kristo kulingana na ufunuo wa siri (Waefeso 1:9-10). Bwana yeye yule mmoja, Yesu Kristo, alitukuzwa kupitia huduma zote mbili.

Jambo ambalo halipaswi kukosewa hapa ni kwamba Mtume Petro na Mtume Paulo hawakujitungia tu wenyewe huduma zao hizo mbili tofauti kutoka hewani. Alikuwa ni Roho Mtakatifu aliyezungumza kupitia wao!

Hivyo, kugawa unabii na ufunuo wa siri, ni kuigawa huduma ya Roho Mtakatifu kwa usahihi.

Roho Mtakatifu Anamshuhudia Yesu

Yesu alisema kwamba wakati Msaidizi atakapoletwa kutoka kwa Baba, atakuwa na jukumu la kumshuhudia yeye:

“Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia” (Yohana 15:26)

Tunapojifunza kuigawa sawasawa kweli ya neno la Mungu, tunajua kwamba, haitoshi tu kushuhudia juu ya Yesu, bali pia ni lazima tuulize swali kuwa, “tunamshuhudiaje huyo Yesu?”

Bwana alielezea kwamba Roho Mtakatifu angehudumu kwa mtindo wake yeye (Yesu) katika huduma yake ya kidunia:

“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana 14:26)

Yesu alikuwa mhudumu kwa watu wa tohara (Warumi 15:8). Naye Roho Mtakatifu, kupitia Mtume Petro, siku ile ya Pentekoste alikuwa ni mhudumu kwa watu wa tohara pia.

Mabadiliko katika Huduma

Wakati Bwana Yesu aliporudi kwa ‘mtesaji’ wake mkuu, Sauli, hakumpa tu neema ‘tele’ juu yake, lakini pia alimpa huduma mpya kutoka kwake.

Alimfunulia Paulo jinsi ya kuhudumu kulingana na SIRI (Warumi 16:25).

“Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo” (Wagalatia 1:11-12)

Siri hii ya Kristo iliifanya huduma ya Paulo kuwa tofauti na huduma ya Petro aliyezungumza mambo yaliyomo katika unabii.

“Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihubiri habari za siku hizi” (Matendo 3:24)

Mabadiliko ya Huduma ya Roho Mtakatifu

Wakati wa Pentekoste, ilikuwa ni Roho Mtakatifu aliyemjaza Petro kuhubiri yale manabii waliyoyatabiri (Matendo 2:4).

Baada ya Bwana wetu, Yesu Kristo kumpa Mtume Paulo huduma tofauti, huduma ya Roho Mtakatifu nayo ilibadilika pia, ili kumshuhudia Yesu Kristo kulingana na ufunuo wa ile siri.

Ilikuwa ni Roho Mtakatifu yule yule aliyemjaza Mtume Paulo kuhubiri siri ya Kristo:

“Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake” (Waefeso 3:1-7)

Alikuwa ni Roho Mtakatifu aliyekuwa anafanya kazi ndani ya Mtume Petro na Mtume Paulo ndiye ambaye ‘alipanga’ mabadiliko kutoka kwenye huduma yake kwa Israeli kwenda kwenye huduma mpya inayohusu Kanisa, Kiumbe Kipya!

Roho Yeye Yule, Huduma Tofauti

Ili tuweze kuigawa vyema ‘Pentekoste’ kutoka kwenye Kanisa Mwili wa Kristo, ni lazima pia tuigawe vizuri huduma ya Roho Mtakatifu.

Haitoshi tu ‘kuiona’ huduma ya Roho Mtakatifu, ni lazima pia tuulize, “anahudumu vipi?” Maana, namna tunavyomhubiri Yesu Kristo imebadilika, kwa sababu Roho Mtakatifu alibadilisha huduma yake kuwa ya Kanisa.

Wakati wa Pentekoste Roho Mtakatifu alihudumu kulingana na unabii. Kupitia kwa Mtume Paulo, Roho Mtakatifu alihudumia siri ya Kristo. Roho yeye yule, huduma tofauti!

Kwa Utukufu Wake Kristo Yesu

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *