Home 2021 June 20 Thamani ya Kujifunza Biblia

Thamani ya Kujifunza Biblia

Thamani ya Kujifunza Biblia

“Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2 Timotheo 3:14-17)

Timotheo alikuwa ni kijana mwenye ‘bahati’. Baba yake hakuwa muumini wa Kristo, lakini mama yake, aliyekuwa mcha Mungu, aliziziba pengo hilo na kumfanya kijana huyo asiwe na ukosefu wa imani, kwani siku baada ya siku, tangu utoto wake wa mapema, mama yake alimfundisha Neno la Mungu. Kama matokeo ya hilo, alibahatika kumjua Kristo katika umri mdogo na baadaye akawa mfanyakazi-mwenza mwaminifu na mshirika wa karibu wa Mtume Paulo katika kuzitangaza “habari njema za neema ya Mungu”

Katika barua yake ya mwisho kabisa Mtume mkuu Paulo anakumbuka “imani isiyo na unafiki…” ambayo ilikaa kwanza kwa nyanya yako Loisi, na mama yako Eunike” (2 Timotheo 1:5):

“Nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo”

Laiti kama tungekuwa na akina mama na bibi wengi wa namna hii leo, na waume wa kuwasaidia! Na kama watoto wetu katika ulimwengu wetu huu wa sasa hawangewekwa kwenye bahari isiyo na utulivu ya uvumi wa wanadamu, badala yake wangefundishwa kweli za milele za Neno la Mungu, Biblia; kama ilivyokuwa kwa kijana Timotheo! Dunia hii ingekuwaje katika maarifa ya Kristo?

Sisi sote tunahitaji “kuyajua Maandiko Matakatifu,” sio tu kwa sababu yanatufundisha kumcha Mungu na kutujengea tabia ya maadili, lakini zaidi ya yote kwa sababu “yana uwezo wa kutuhekimisha hata tupate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.”

Mada ya Biblia, Agano la Kale pamoja na Jipya, ni Bwana Yesu Kristo, ambaye utajiri wa neema yake inayookoa umefunuliwa kwetu katika Nyaraka za Mtume Paulo, mkuu wa wenye dhambi waliookolewa kwa neema. Ilikuwa ni Mtume Paulo ambaye Mungu alimkabidhi mahubiri ya msalaba wa Kristo. Yeye ndiye anayetuambia juu ya utajiri unaobubujika kutoka Kalvari. Yeye ndiye anayetuambia, kwa uvuvio wa kimungu kwamba:

“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7)

“Ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu” (Waefeso 2:7)

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *