Home 2021 May 28 Bwana Mmoja, Imani Moja, Batizo Tatu!

Bwana Mmoja, Imani Moja, Batizo Tatu!

Bwana Mmoja, Imani Moja, Batizo Tatu!

Kwa kuwa Paulo anaweka wazi kuwa kuna ubatizo mmoja tu katika Waefeso 4:5, kwa nini kuna malumbano mengi juu ya ubatizo?

Kama Paulo anasema kuna ubatizo mmoja tu basi lazima iwe ni huo ubatizo ambao yeye Paulo anaufundisha. Ubatizo huu unapatikana katika 1 Wakorintho 12:13 na Warumi 6:3:

“Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja”

“Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?”

Ubatizo huu ni ‘mkavu’, hauna maji, na unafanywa na Roho akitubatiza (akituzamisha) katika Kristo. Huu ndio ubatizo unaotuokoa leo. Sio ubatizo wa maji wa aina yoyote ile (mengi au machache).

Kama umeweza kuliona hili, basi umefanikiwa kuruka hatua moja mbele, kuelekea uelewa wa maandiko kwamba habari ambayo Yesu alimpa Paulo inachukua nafasi ya habari zinazopatikana katika Mathayo, Marko, Luka na Yohana

Ikiwa umeshindwa kuliona hili, basi utakuwa umekwama katika juhudi zako za kujaribu kupatanisha batizo nyingi zilizofundishwa katika huduma ya Bwana katika mwili hapa duniani dhidi ya ubatizo mmoja aliyoufundisha Paulo katika Waefeso 4:5.

Mathayo 3:11 ni tofauti kabisa na Waefeso 4:5:

“Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto

Katika aya hii kuna ubatizo wa aina tatu: (1) ubatizo wa maji kwa toba; (2) kubatizwa na Roho Mtakatifu; na (3) ubatizo na moto.

Orodha hii haijumuishi ubatizo wa Bwana wetu Yesu Kristo, katika mistari minne tu baadaye (Mathayo 3:15), ambayo haingeweza kuwa ni kwa ajili ya toba kwa sababu Yesu hakuhitaji kutubu. Ubatizo wake ulifanywa ili ‘kuitimiza haki yote’.

Unaweza ukawa umebatizwa katika maji mengi, lakini Je! umebatizwa na Roho Mtakatifu? Unao ujasiri wa kusema umefanywa hivyo? Na, Je! Umebatizwa kwa moto? Nadhani hili usingelipenda (Mathayo 3:12; Isaya 4:4).

Linapokuja suala la ubatizo tunakabiliwa na hitaji la maandiko. Je! Tunaweza kukubali kwamba Yesu alimfunulia Paulo habari ambayo ilichukua nafasi/mahala pa mafundisho ya awali juu ya ubatizo?

Au tunaamini kwamba Paulo alikosea; na kwamba kuna zaidi ya ubatizo mmoja; wakati ubatizo ule ambayo Yesu alibatizwa nao sisi hatuwezi kamwe kuufanya/kubatizwa nao!

Kama kanisa leo lingetambua ufunuo endelevu uliotolewa na Kristo kwa Paulo, basi kusingekuwa na kuchanganyikiwa hata kidogo juu ya ubatizo. Tungeweza kuelewa kusudi la batizo zote kumi na mbili zilizopo katika maandiko na bado tungehitimisha kwamba Kristo alikuwa yuko sawa wakati anamfundisha Paulo:

“Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja” (Waefeso 4:5)

Kwa Utukufu Wake Yesu Kristo

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *