Home 2021 May 10 Kutembea Katika Roho Kabla ya Paulo

Kutembea Katika Roho Kabla ya Paulo

Kutembea Katika Roho Kabla ya Paulo

Watumishi wengi wa Mungu, wanaoichukulia Biblia kikawaida (yaani wale waliokosa maarifa ya kuigawa kweli ya neno la Mungu sawasawa), kwa kawaida/wakati wote ‘wanavimba na kutaka kupasuka kwa hasira’ wakisikia kwamba Mtume Paulo alifundisha ujumbe tofauti na wale mitume kumi na wawili, waliokuwepo kabla yake.

Ni jambo la kushangaza kidogo kuona kwamba watumishi hao pia wanazungumzia juu ya umuhimu wa mwamini kutembea katika Roho.

Kwa nini jambo hilo ni la kushangaza? Kwa sababu ni Mtume Paulo tu ndiye anayeeleza na kufafanua maana ya kutembea katika Roho!

Kabla ya Roho

Roho Mtakatifu hakutumwa kutoka mbinguni mpaka baada ya Kristo kufa, kuzikwa, kufufuka, na kupaa kwake mbinguni. Kwa ukweli huu peke yake isingewezekana kwa mtume yeyote kabla ya Pentekoste kutembea katika roho, bila kuwa na huyo Roho.

Ni vyema ikifahamika hapa kuwa hata huduma ya Yesu Kristo hapa duniani haikujumuisha maagizo juu ya jinsi ya kutembea katika Roho. Badala yake, Yesu alizungumzia juu ya utunzaji wa sheria, ahadi za baadaye, na unabii.

Je! Wangewezaje wale mitume kumi na wawili, katika Mathayo mpaka Yohana, kufundisha ujumbe sawa na Paulo juu ya kutembea katika roho, wakati hao kumi na wawili hawakuwa na Roho bado?

Roho wa Agano Jipya

Yesu aliithibitisha ahadi ya kuja kwa Roho Mtakatifu (Warumi 15:8; Luka 24:49), lakini kuja kwa Roho ‘katika nguvu’ ni tofauti na kujifunza jinsi ya kutembea ‘katika roho’ chini ya neema.

Kulingana na unabii, ilikuwa ni lazima Israeli ipokee Roho wa Mungu ili ifanye kazi ndani ya agano lao jipya (Yohana 3:7; Ezekieli 36:26).

Nyaraka za Kiebrania ziliandikwa na mitume kwa Israeli wakiwa wamejazwa na Roho Mtakatifu; lakini nyaraka hizo pia ziko kimya juu ya jinsi ya kutembea katika Roho.

Ni ukweli usiopingika kwamba, wanazungumza juu ya kuwa na Roho, nguvu ya Roho, na kumkataa Roho; lakini jinsi ya kutembea katika Roho ni jambo/mada ambayo hawashughuliki nayo – yaani, hawajaifafanua!

Badala yake, Yakobo anasema, “Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale” (Yakobo 2:22)

Yohana anasema upendo wa Mungu umekamilika kwa wale wazishikao amri zake (1 Yohana 2:4-5).

Kama hautembei katika Roho kama maagizo ya Paulo yalivyo, basi kimsingi wewe unatembea kwa kufuata mwili, upo katika maagano, na hakika upo chini ya sheria.

Hii ndiyo sababu Paulo aliwaambia Wagalatia ambao walikuwa wakishawishiwa na watunza sheria wa Kiyahudi, maneno haya: “Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?” (Wagalatia 3:3).

Kutembea katika Roho

Maagizo juu ya jinsi ya kutembea katika Roho hupatikana katika nyaraka za Paulo pekee, ambazo ni Warumi na Wagalatia.

Ni Paulo tu anayeandika juu ya kutembea katika Roho, kwa sababu yeye ndiye mtume maalum wa kipindi cha neema ya Mungu.

Chini ya neema ya Mungu, kwa mara ya kwanza, watu ambao hawako chini ya sheria, wala hawakuwa chini ya maagano, na sio Waisraeli katika mwili; sasa wanaweza kupokea Roho wa Mungu (Waefeso 2:18; 1 Wakorintho 12:13):

“Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja”

“Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja”

Kwa kuwa ni majira ya neema, imefunuliwa pia jinsi ya kumpokea Roho Mtakatifu bila agano, na jinsi ya kutembea bila sheria:

“Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho” (Wagalatia 5:25)

Ingawa watumishi wengi katika kanisa leo wanapinga wazo la kuigawa huduma ya Petro (unabii) na huduma ya Paulo (siri) na kuubali ukweli kwamba Paulo alikuwa na ujumbe tofauti na wale kumi na wawili, kila wakati watumishi hao wanapohubiri juu ya kutembea katika Roho wanashuhudia na kuthibitisha usahihi wa mgawanyo huo.

Bila ya kufunuliwa kwa siri ya Kristo, hakuna hata mtu mmoja kati yetu leo, angejua jinsi ya kutembea katika Roho.

Tambua kwamba kutembea katika Roho halikuwa jambo ambalo watu waliambiwa linafanywaje kabla ya Paulo!

Kwa Utukufu Wake, Kristo Yesu.

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *