Home 2021 May 06 Laana ya Zaka

Laana ya Zaka

Laana ya Zaka

Chini ya agano la wajibu na Israeli, Mungu aliwabariki wale tu waliozishika amri na kuwalaani wale ambao hawakuwa watiifu.

Hii ndiyo sababu Paulo anatangaza kuwa chini ya sheria kulikuwa na laana kwa watu wenye dhambi kwani hata kwa kosa moja kulikuwa ni uvunjaji wa agano:

“Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye” (Wagalatia 3:10)

Yakobo naye aliyaelezea mahitaji haya magumu ya sheria kwa kuandika maneno haya:

“Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote” (Yakobo 2:10)

Wakati wa huduma yake kwa watu wa tohara, Yesu hakuifuta sheria. Badala yake alielezea zaidi uwezo wa sheria kulaani:

“Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 5:19)

Kwamba sheria ya Mungu ilihitaji zaka na dhabihu, ni jambo lililo wazi kabisa (Kumb. 14:22):

“Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka)

Kilichopata umaarufu zaidi kwa ‘wahubiri’ wa zaka ni ule ‘mkemeo’ wa Mungu kwa Israeli kwa ukosefu wao wa kutoa zaka na dhabihu (matoleo):

“Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu” (Malaki 3:8)

Kimsingi, Israeli iliwekwa (sio ‘ingewekwa’ kana kwamba ni wakati ujao) chini ya laana kwa kuvunja makubaliano ya agano:

“Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote” (Malaki 3:9)

Maneno ya Paulo juu ya taifa la Israeli kuwa chini ya laana, yanapata nguvu (kuwa ni ya kweli) pale tunasoma juu ya hukumu hii kwao!

Hatupo Chini ya Laana

Kihistoria, Wakristo wameshindwa kufikia mahitaji ya sheria ya zaka kwa kutoa kidogo sana kuliko kile hiyo sheria ya Mungu inavyotaka kwa Israeli (ukisoma kwa uangalifu utagundua kuwa hata hiyo 10% haitoshi).

Ingawa ukosefu wa ukarimu unaweza kuwa shida kanisani, shida mbaya zaidi hutengenezwa kila mwaka na ‘ukuhani’ wa makanisa ya kisasa ambayo huwaweka waumini wao chini ya laana ya zaka. Hakuna jambo lililowazi kabisa kama hili, kwamba mazoea haya ya kila mwaka ni makosa makubwa mbele za Mungu.

Tunajifunza kutoka kwa Mtume Paulo kwamba hatupo tena “chini ya sheria” na kwamba tuko huru kutoka kwenye vifungo vyake (Wagalatia 4:9). Zaidi sana, Yesu Kristo alitukomboa kutoka kwenye laana ya sheria:

“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti” (Wagalatia 3:13)

Kumuweka mtu chini ya mfumo wa kutoa zaka na kutoa sadaka kama inavyotaka sheria ya Musa ni sawa na kupuuza ukombozi wa Kristo Yesu msalabani na kulirejesha Kanisa nyuma na kuliweka chini ya laana ya sheria.

Wale wanaoishi chini ya uhuru na neema ya Mungu hawawezi tena kuwekwa chini ya laana (Wagalatia 5:1):

“Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa”

Kutoa zaka ya lazima sio ‘desturi’ ya kanisa, Mwili wa Kristo. Wale wote wanaofundisha kutoa zaka wanathibitisha ukweli kuwa hawajui maagizo ya Mtume Paulo kwa Kanisa na zaidi sana wanafundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu (Tito 1:11).

Ukarimu wetu ni upeo wa shukrani zetu kwa Mungu kwa kile alichofanya msalabani. Wakati wachungaji wanapotumia sheria kuhamasisha utoaji, kimsingi kwa kufanya hivyo, wanakataa nguvu zote kutosha ‘zinazotosha’ za neema ya Mungu (2 Wakorintho 9:7-8):

“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema”

Na huo ndio moyo wa Mungu katika UTOAJI, hata katika sheria:

“Bwana akanena na Musa, akamwambia, Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu” (Kutoka 25:1-2)

Kwa utukufu wa JINA, lipitalo majina yote!

Author: Festus Patta

5 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *