Home 2020 August 28 Pasaka: Injili Yenye Msalaba

Pasaka: Injili Yenye Msalaba

Pasaka: Injili Yenye Msalaba

Wakati tukiwa kwenye sherehe za kuazimisha sikukuu ya Pasaka, kama habari njema ya ukombozi kwa wanadamu wote; ni vyema pia tukajua ni nini hasa tunachokisema maana kwenye Biblia kuna ‘habari njema’ za aina nyingi na pia hazifanani kwa kila mtu!

Yesu, katika huduma yake hapa duniani, alifundisha injili ya ufalme. Habari njema ilikuwa kwamba ule ufalme uliohaidiwa muda mrefu kwa taifa la Israeli hatimaye “umekaribia”, ulikuwa “karibu” (Marko 1:14-15).

Injili Bila Msalaba

Wokovu kulingana na injili ya ufalme ulimaanisha ukombozi kutoka kwenye mikono ya watawala waovu wa ulimwengu huu. Watu wa Mungu, na mataifa maaminifu, wangetawaliwa na Masihi wa Mungu katika utii kwa taifa la Israeli.

Jambo lililo hakika ni kwamba injili ya ufalme haikuhitaji ufahamu wa msalaba wa Kristo, achilia mbali kujua kusudi lake! Katika Luka 9:1-2 Yesu akawapa uwezo wanafunzi wake na kuwatuma wautangaze ufalme, lakini sura tisa baadaye Yesu anawaambia kuwa imempasa kufa, nao hawakuelewa chochote; jambo hili lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa (Luka 18:34). Kuhubiri injili ya ufalme, ni kutangaza habari njema iliyokosa msalaba.

Injili yenye Msalaba

Hata hivyo, injili ya Paulo ni habari njema inayohubiri kazi timilifu na toshelevu ya msalaba wa Kristo (1 Wakorinto 15:1-4). Wanafunzi wa Yesu (Thenashara) walikuwa ‘wajinga’ wa injili ya msalaba; ingawa kuhubiriwa kwa msalaba ni nguvu ya Mungu iletayo wokovu kwa Kanisa leo (1 Wakorinto 1:18)

Mungu haleti ufalme kwa Wayahudi leo, bali anahubiri habari njema ya Kristo aliyesulubiwa na kufufuka kwa ajili ya dhambi za watu wote. Injili iliyokosa msalaba, ni injili isiyoweza kuokoa wenye dhambi; Injili pekee inayookoa leo, inauhitaji msalaba wa Kristo bila nyongeza yoyote!

Kwa Utukufu Wake Kristo

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *