Ndoa

Ndoa

“Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.  Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Mathayo 19:6)

Mungu huona ndoa kuwa jambo muhimu sana, zaidi ya kuwa tu ni mkataba kati ya watu wawili. Ni muungano mtakatifu kati ya mwanamume na mwanamke, uliowekwa na Mungu tangu mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwengu. Biblia inasema hivi:

“Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe” (Marko 10:6-9; Mwanzo 2:24)

Maneno “alichokiunganisha Mungu” hayamaanishi kwamba Mungu ndiye huwachagulia watu wenzi wa ndoa; bali Mungu ndiye Mwanzilishi wa mpango wa ndoa, na Biblia inakazia uzito wa muungano huo. Kwa hiyo, wenzi wa ndoa ambao huona ndoa kuwa muungano mtakatifu na wa kudumu hujitahidi sana kufanya ndoa yao ifanikiwe. Hivyo, wao hufanikisha ndoa yao kwa kutafuta mwongozo wa Biblia kuhusu jinsi wanavyoweza kutimiza madaraka yao wakiwa mume au mke.

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *