Home 2021 October 19 Rehema Kwa Wote!

Rehema Kwa Wote!

Rehema Kwa Wote!

Je! Umewahi kujiuliza ni kwa namna gani ulimwengu wa kipagani ulifikaje hapa ulipo sasa?: kuabudu ‘sanamu’,  kushikwa na woga mwingi juu ya ushirikina, na mabaya mengine mengi unayoyajua?

Biblia inayo majibu hayo katika Waraka wa Paulo kwa Warumi. Mara tatu katika Sura ya kwanza tunasoma juu ya Mungu ‘kuuacha’ ulimwengu wa watu wa Mataifa wafanye watakavyo: “Mungu aliwaacha…(24), Mungu aliwaacha…(26), Mungu aliwaacha…(28)” Kwa nini? Kwa sababu hao Mataifa walimwacha Yeye:

“Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao”

“Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili”

“Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”

Yote haya ni matokeo ya asili ya kuachana na Mungu na Neno Lake. Hata hivyo, lipo tumaini na hakikisho na furaha aliyowekewa mtu yeyote ambaye atatii ujumbe wa Mungu – haswa katika Kitabu cha Warumi. Ni katika kitabu hicho ndimo tunamosoma jinsi Myahudi alivyojiunga na Mmataifa katika kumkataa Kristo, na Mungu kwa sababu hiyo, ilimbidi awaache wote.

Sikiliza ushuhuda huu kutoka kwa Warumi 11:32:

“MAANA MUNGU AMEWAFUNGA WOTE PAMOJA KATIKA KUASI ILI AWAREHEMU WOTE”

Ndio kusema, ALIWAACHA Wayahudi na Mataifa ili AWEZE kuonyesha neema Yake kwa watu wote ambao wanaweza kumrudia Yeye kwa imani katika Kristo, na hivyo kuwapatanisha wote wawili (Waamini wa Kiyahudi na wa Kimataifa) kwake Yeye mwenyewe katika mwili mmoja, kwa msalaba (Waefeso 2:16).

Kwa Utukufu Wake Kristo Yesu

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *