Home 2022 January 25 Je! Tukae Kimyaaa…?

Je! Tukae Kimyaaa…?

Je! Tukae Kimyaaa…?

Katika kila nyakati, Mungu daima, amekuwa na watoto wenye nia njema ambao walimtumikia Yeye kwa unyofu wa moyo lakini bila ya kuwa na ufahamu wa Neno Lake lililogawanywa kwa usahihi, na hivyo wakafanya na kufundisha mambo ambayo yalikuwa mabaya (hayakuwa sawasawa na wakati au kipindi husika).

Lakini katika kila enzi pia, kumekuwa na watu kama “wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende…” (1 Mambo ya Nyakati 12:32), wasawazishaji waliojua mahali waliposimama katika mpango wa Mungu, na hivyo walijua jinsi ya kufanya kile ambacho kilikuwa sawasawa na wakati au kipindi husika.

Hivyo, hatupaswi kuona haya kutangaza bila woga kwamba, katika kipindi hiki cha sasa cha majira ya neema; sisi waumini wa neema ya Mungu, ni wana wa siku hizi wa Isakari! Tuna ufahamu wa nyakati! Tunajua kile ambacho Mwili wa Kristo unapaswa kufanya.

Lakini kwa ujuzi huo mkubwa, huja wajibu mkubwa pia! Kwa nini basi usiingie kwenye vita hivi, vikubwa pia, vya kuutafuta na kuutetea ukweli huu wa Injili ya Neema ya Mungu? TAMBUA, sio kile unachokijua ndicho chenye umuhimu, bali ni kile “unachokifanya” (Wafilipi 4:9) na hicho unachokijua…

Je! Tukae tuendelee kukaa kimya hata kama kuna makosa? HAPANA! Hebu tufanye kitu sasa, huku tukijua kwamba tunachofanya kiko sahihi…

Sifa na Uweza na Ukuu Vina Yeye Milele Yote; AMINA.

Author: Festus Patta

6 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *