Home 2024 March 05 SAA ILE!

SAA ILE!

SAA ILE!

Historia imerekodi matukio mengi makubwa na muhimu, lakini hakuna kati ya hayo, linalokaribiana kwa muhimu kama kusulubiwa kwa Kristo Yesu juu ya msalaba wa Kalvari. Akiurejelea wakati huu, kipindi hicho ukiwa wakati ujao, wakati jambo hili lingetukia, Bwana wetu alisema tena na tena juu ya “saa,” “saa ile” na “saa yangu,” na ndivyo yasemavyo Maandiko  matakatifu.

Wakati adui zake walipotoka kumpiga kwa mawe, kwenye Sikukuu ya Vibanda, maandishi yanasema tu: “Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado” (Yohana 7:30).

Hatimaye, wakati huo wa kutisha ulipofika, tunasoma:

“Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye” (Luka 22:14).

“Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.” (Yohana 12:23-24).

“Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii” (Yohana 12:27).

“Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo” (Yohana 13:1).

Mwishowe, katika sala yake kuu ya ukuhani mkuu, iliyotamkwa katika kivuli cha msalaba, “akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe” (Yohana 17:1).

Hii ndiyo saa ambayo kwayo, dhabihu na unabii mwingi wa Agano la Kale, ulikuwa umeelekezwa…

Hii ndiyo saa ambayo kwayo, waliokombolewa wote, wataitazama nyuma kwa shukrani na sifa kwa nyakati zote zijazo…

Hakungekuwa na wokovu kwa wenye dhambi bila saa hii, wala tumaini lolote la dunia iliyorejeshwa (mpya) na laana ya dhambi kuondolewa…

Mungu ni wa kushukuriwa daima, kwa sababu Kristo Yesu alikuwa tayari kukabiliana na SAA HII ya kutisha, nasi kwa hiyo, “tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7).

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *