Home 2024 March 01 TASWIRA YA MPUMBAVU!

TASWIRA YA MPUMBAVU!

TASWIRA YA MPUMBAVU!

Watu wasioamini kwamba kuna Mungu, wanalalamikaga kwamba Wakristo wanazo sikukuu nyingi za kusherekeha; Nasi tunapenda kuwajibu kwa kutaja kwamba Aprili 1 ni Siku yao ya Wakana-Mungu, kwa maana Maandiko yanasema “mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu” (Zaburi 14:1; 53:1)! Lakini hata hivyo, hili sio jambo la kufurahisha, hasa pale watu wa Mungu wanapojifanya wajinga!

Kwa miongo kadhaa sasa, familia yetu hii ya Kikristo imekuwa katika kitendawili kikubwa hasa katika msimu ule maarufu wa Krismasi. Kwetu sisi, msimu huo, ni tukio lenye kumbukizi maalumu. Na zaidi ya hayo, unatuhimiza tutenge muda nje ya ratiba zetu zenye shughuli nyingi za kila siku, ili kutumia muda huo pamoja, na katika kutembeleana na kubadilishana zawadi. Lakini pamoja na hayo, pia kuna hali ya kutumainisha kwani, siku baada ya nyingine, na kwa kadiri ya vipande vya ‘mafumbo’ vinavyoongezwa; tunaona taswira iliyo wazi ikijitokeza. Kwamba, katika Kitabu cha Mithali, Mungu anatupatia taswira hiyo iliyo wazi, ingawa isiyopendeza, ya mtu mpumbavu…

Mtu mpumbavu, anaweza kutambuliwa kwa urahisi, kwa angalau sifa takribani kumi zilizoelezwa na Mfalme Sulemani, kwamba:

Mpumbavu “hukataa maonyo” kwa hasara ya nafsi yake yeye mwenyewe (15:32a). Ataziba masikio yake kusikiliza pale anapopewa ushauri wa busara…

Midomo ya mpumbavu “huingia katika fitina”, na kinywa chake “huita mapigo”. Kinywa cha mpumbavu ni “uharibifu wake”, na midomo yake ni “mtego wa nafsi yake” (18:6-7). Kwa kawaida, mpumbavu huwa anatafuta shida, na kwa kawaida huwa ni mjeuri katika maneno yake…

Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo, na yeye “asingiziaye” ni mpumbavu (10:18). Kuhamisha lawama kwa wengine huwa ndio mtindo wake wa maisha, kama mwavuli wa makosa yake…

Njia ya mpumbavu “imenyoka machoni pake mwenyewe” (12:15), na kwake yeye mpumbavu huyo, “kutenda maovu ni kama mchezo” (10:23). Yeye hudhani kwamba, wakati wote yuko sahihi na kwamba kwake hakuna makosa…

Mpumbavu “hueneza upumbavu wake” (13:16b), na mpumbavu huyo anafanya hivyo kwa sababu “mpumbavu ana ufidhuli na kujitumai” (14:16b). Ni kama vile mtu mmoja alivyowahi kusema kwamba: “Ni afadhali kudhaniwa kuwa ni mjinga, kuliko kufungua kinywa chako na kuyaondoa mashaka hayo…”

Mithali pia huwasilisha dhana kwamba mpumbavu “hatasikiza maonyo”, hata kama atapigwa mapigo mia (17:10); Mithali pia huzungumza juu ya mpumbavu “anapopaswa kusikiliza” (17:28); Sikuzote, mpumbavu “huchochea ugomvi” (20:3), na kwamba mpumbavu “hudhihirisha hasira yake yote” (29:11). Huyo, anaonekana kuwa kama ni mtu aliye “bize kuharibu” na ambaye hufurahia kuendelea “kukwaluzana” na “kujiingiza” katika “migogoro isiyokoma” na wengine…

Kwa kadiri tunapoitazama kwa makini picha hii ya mpumbavu, kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza kama tuna mojawapo ya sifa hizi zilizoelezwa. Ikiwa ndivyo, tunakuhimizwa tufanye jambo ili kujirekebisha juu ya hilo. Chukua moja au mawili kati ya haya mazoea unayojua unahitaji kuyafanyia marekebisho, na umwombe Bwana akuwezeshe kubadili mtindo wako wa maisha, kisha mwombe mpendwa wako akujibike katika eneo hili; na katika kufanya hivyo, mruhusu Mungu akubadilishe…

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *