Home 2024 January 28 KITABU CHA KWANZA KUSOMA!

KITABU CHA KWANZA KUSOMA!

KITABU CHA KWANZA KUSOMA!

Katika miaka iliyopita, maisha yalipokuwa sahili, watu walikuwa na wakati mwingi zaidi wa kutafakari juu ya maswali muhimu ya hatima ya maisha: Maswali kama vile – Nini kitatokea kwangu wakati nitakapokufa? Je, kuna mbingu?; Je, kuna kuzimu? Je, naweza kumjua Mungu? Je, Mungu anaweza kunisamehe dhambi zangu? Kama ndiyo, ni kwa msingi gani? Na je, nifanye nini ili niokoke?

Uchu wa mali, biashara na maendeleo ya teknolojia ya siku zetu hizi, hata hivyo, vimeyasonga maisha yetu na kusababisha ugumu kiasi kwamba matatizo yasiyo kuwa ya msingi, yamewanyima watu wengi, uwezo wa kufikiria yale yaliyo muhimu zaidi; hata wakati wakiwa katika kupumzika!

Hata hivyo, pamoja na harakati na wasiwasi nyingi, kelele kutoka pande zote na kukengeushwa kwingi; Zipo roho zilizofadhaika, zenye njaa na kiu ya maridhiko ya kweli, zenye kuhitaji usafishwo wa dhati kutoka kwenye dhambi, na zenye kuhitaji ukombozi thabiti kutoka kwenye mzigo mbaya wa dhamiri yenye hatia…

Watu kama hao, wanapaswa kusoma Waraka wa Paulo Mtume kwa Warumi na kutafakari juu ya ujumbe wake mkuu wa wokovu. Kwa HAKIKA; Hiki ndicho kitabu cha kwanza, wanachopaswa kusoma.

Katika Waraka kwa Warumi, Mtume aliyevuviwa na Roho Mtakatifu anatangaza kwamba “wote wamefanya dhambi” (3:23) na kwamba “mshahara wa dhambi ni mauti” (6:23a). Huu sio mwisho ya yote, kwa kuwa katika Warumi pia kumetangaza habari njema kwamba Bwana Yesu Kristo “alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuka ili tupate kuhesabiwa haki” (4:25) ili kwamba, kwa sababu hiyo, tuwe na “amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo” (5:1).

Zaidi ya hayo, katika Warumi hutangazwa neema isiyokifani kwa wale wote wanaomwamini Kristo. “Sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa zaidi, lakini dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi” (5:20). Hivyo waamini “wanahesabiwa haki bure kwa neema [ya Mungu], kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu” (3:24) na “zawadi [ya bure] ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (6:23b).

Tunawasihi wale wote ambao hawana uhakika wa wokovu, wasome kwa makini na kwa maombi Waraka huu mkuu kwa Warumi. Kwa HAKIKA, ukifanya hivyo, utamshukuru Mungu kwa maisha yako yote ya hapa duniani – na ya yale ya umilele; kwamba ulifanya hivyo!

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *