Home 2023 December 24 “MTOTO YESU” Vs “BWANA WA UTUKUFU”!

“MTOTO YESU” Vs “BWANA WA UTUKUFU”!

“MTOTO YESU” Vs “BWANA WA UTUKUFU”!

Kila mwaka, wakati wa Krismasi, “mtoto Yesu” ni mada ya mahubiri, mazungumzo, majadiliano, mazingatio na mengine mengi. Kwa hakika, mwaka mzima, Mtoto mchanga mikononi mwa mama yake na Msulubiwa aliyekufa msalabani huwekwa daima mbele ya makusanyiko, huku ufufuko wa Bwana wetu, kupaa kwake na utukufu wake wa sasa huko mbinguni unawekwa mbele ya makusanyiko hayo kwa uchache sana. Hii ni kwa sababu ni wachache sana ambao wamezingatia ujumbe mkuu wa Mtume Paulo kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo aliyetukuzwa mbinguni. Katika 2 Wakorintho 5:16, Mtume huyo ameandika:

“Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena”

Inasikitisha kwamba wapendwa wengi bado wanamjua tu “Kristo kwa jinsi ya mwili.” Wanapenda sana kujadili “habari za injili” kuhusu “Mtu yule wa Galilaya,” na kujikuta wamekuwa wageni kabisa katika Nyaraka kuu za Mtakatifu Paulo.

Paulo alikuwa mtume kwa ajili ya “wakati huu wa sasa wa neema ya Mungu.” Ni yeye ndiye anayemleta kwetu Kristo katika utukufu wake wa sasa kama Mgawaji (Dispenser) mkuu wa neema ya ukombozi, kwa njia ya usitahilisho (sifa) alioshinda pale Kalvari. Katika Waefeso 1:17-23 tumeandikiwa kwa ajili yetu, maombi ya Mtume Paulo, ili tupewe “roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua Kristo” ili tufikie uzoefu wake…; Anaomba:

“Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;

“Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;

“Na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;

“Aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

“Juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;

“Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo

“Ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”

Hima tumshukuru Mungu sote kwamba mtoto Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na akawa Mwokozi aliyefufuka, aliye hai kwenye mkono wa kuume wa Mungu, ambaye kweli kweli, “aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee” (Waebrania 7:25).

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *