Home 2023 December 12 JE! YESU ALIWATUKUZA MAFARISAYO?

JE! YESU ALIWATUKUZA MAFARISAYO?

JE! YESU ALIWATUKUZA MAFARISAYO?

Katika kuihubiri Neema ya Mungu iliyogawanywa sawasawa, HAIKO namna ya KUMKWEPA Mtume Paulo na NYARAKA zake. Na katika kufanya hivyo, hutokosa kutuhumiwa kwamba ‘unamtukuza sana Paulo kuliko Bwana Yesu au unamwinua Paulo juu ya Kristo’. Kwa wale wasioijua Neema ya Mungu na uwakili wake, hili linaweza kuwa tatizo kwao, lakini kwa wabobevu hilo ni AGIZO na inawapasa kuwahimiza waumini wote kumfuata Paulo, kama yeye alivyomfuata Kristo (1 Wakorintho 11:1):

“MNIFUATE MIMI KAMA MIMI NINAVYOMFUATA KRISTO”

Hatumtukuzi Paulo, na tunaweza kuthibitisha hilo! Je! Unakumbuka wakati Bwana Yesu aliposema maneno haya?

“Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda” (Mathayo 23:1-3a)

Je! Bwana wetu, Yesu Kristo alikuwa akiwatukuza waandishi na Mafarisayo pale alipowaagiza wanafunzi wake wazingatie maneno yao? La hasha! Je, alikuwa ‘akiwainua’ kumpita yeye mwenyewe? Dhairi shairi; HAPANA! Bali alikuwa akionesha tu kwamba viongozi hao wa kiroho wanapaswa kufuatwa kwa sababu walifundisha Sheria ya Musa, na Sheria hiyo ndiyo ilikuwa ni mpango wa Mungu kwa wakati huo. Mpango wa Mungu leo ni mpango wa neema, na huku siko kumtukuza Paulo kwa kusema kwamba yeye ndiye mtume ambaye huduma ya neema ilikabidhiwa kwake (Waefeso 3:1-5):

“Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho”

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *