Home 2023 December 10 KUKOSA UTII

KUKOSA UTII

KUKOSA UTII

“Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo. Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua; ninyi mlioipokea torati kwa agizo la malaika msiishike. Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno” (Matendo ya Mitume 7:51-54)

Mafarisayo na Masadukayo hawakuwa viongozi wa kijeshi, lakini walikuwa na askari fulani wa Kirumi waliokuwa ndani ya himaya yao. Pamoja na  kuwasaidia viongozi wa kiroho wa Israeli, wajibu wao wa kwanza wa askari hao ulikuwa ni kujitiisha kwa heshima kwenye matakwa ya wakuu wao wa Kirumi. Kwa muktadha huo huo, wajibu wa viongozi wa kidini wa Israeli ulikuwa ni kutii yote ambayo Mungu aliamuru katika Neno Lake. Hata hivyo, baada ya ufufuko wa Mwokozi wetu, Kristo Yesu; tunaona katika Matendo 7:51-54, viongozi hawa wa kidini wakiendelea kutenda kwa kutotii Sheria yao ya Musa yenye kustahiwa, Yehova, na Bwana Yesu Kristo.

Wakati Stefano alipotoa taswira ya kihistoria ya ukaidi na upotovu wa makusudi uliokithiri wa Israeli ulioanzia kwa wazee wao wa kwanza, aliwaambia, “Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, sikuzote mnampinga Roho Mtakatifu; Ni yupi kati ya manabii ambaye baba zenu hawakumtesa? Na wamewaua wale waliotangaza kabla ya kuja kwake Mwenye Haki…” (mstari wa 51-52)? Kwa kusikia simulizi hili lisilopingika la wakati uliopita juu ya dhambi ya Israeli, viongozi hawa wa Israeli walipaswa kuitikia ukweli huu kwa utii wa haraka, wakimgeukia Bwana Yesu kwa imani. Lakini badala yake, waliifanya mioyo yao kuwa migumu zaidi. Pamoja na ukweli kwamba, “…walichomwa mioyoni mwao…”, lakini wao “wakamsagia [Stefano] meno yao” (mstari wa 54). Kama ilivyokuwa kwa watangulizi wao, “hawakusikiliza, wala kutega masikio yao” (Yeremia 7:24). Watu hawa “wakafanya masikio yao kuwa mazito, na kufumba macho yao…” (Isaya 6:10), “Naam, walifanya mioyo yao kama jiwe gumu, wasije wakasikia…” (Zekaria 7:12).

Vifungu kama hivi vinapaswa kusababisha kila nafsi kufikiria jinsi inavyoitikia kwa Bwana na kwa Neno Lake. Roho Mtakatifu anapouhakikisha moyo wako, je, unanyenyekea kwa utiifu wa mara moja, au unaufanya moyo wako kuwa mgumu na kuondoka bila tofauti na ulivyokuwa hapo awali? Mruhusu Mungu akubadilishe kwa kutekeleza jambo fulani kutoka kwenye Neno Lake katika vitendo kila iitwapo leo!

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *