Home 2023 December 03 MUNGU: Hakimu Mwenye Haki

MUNGU: Hakimu Mwenye Haki

MUNGU: Hakimu Mwenye Haki

Jinsi hukumu za Mungu zilivyo za haki! Katika Warumi 2:16 Mtakatifu Paulo anasema: “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.” Angalia kwa umakini sana, kwamba hii inahusisha nini:

  1. Atazihukumu “siri za wanadamu.” Katika mahakama za kibinadamu, mahakama za kidunia, mara nyingi kuna upotoshwaji wa haki kwa sababu ukweli wote hauelezwi wazi. Lakini katika “Kiti cha Enzi, Kikubwa, Cheupe” kutakuwa na Hakimu mwenye “macho… kama mwali wa moto” (Ufunuo 19:12), ambaye mbele yake hakutakuwa na siri ambayo inayoweza kubaki kuwa imefichwa (Angalia pia Waebrania 4:13).
  2. Atazihukumu siri za wanadamu “kwa Yesu Kristo.” Sio Baba, bali Mwana ndiye atakayesimamia hukumu ya wasiookolewa. Yohana 5:22 hutangaza kwamba “Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote” na Mstari wa 27 unaongeza kusema kwamba Baba amempa Mwana mamlaka hayo ya kufanya hukumu “kwa sababu Yeye ni Mwana wa Adamu.” Hii inahakikisha hukumu ya haki, kwa maana, wanadamu watahukumiwa siku hiyo na Yule aliyewapenda upeo (vya kutosha) hata kufanyika mwanadamu ili apate kuwa sawa na mwanadamu ili aweze kuwasaidia, na hata kufa kwa ajili ya dhambi zao.
  3. Atazihukumu siri za wanadamu kwa Yesu Kristo “kulingana na injili yangu,” amesema Mtume Paulo. Ni kwa namna gani jambo hili lilivyo la haki, haki yenye hadhi! Kama angewahukumu watu kulingana na sheria ya Musa hakuna mtu ambaye angeokolewa, kwa maana sisi sote tumeivunja Sheria hiyo. Zaidi ya hayo, wana wa Adamu walioanguka, kwa sababu ya asili yao ya uovu (potovu), hawawezi kushika Sheria hiyo kila mara. Hivyo hawatahukumiwa kwa msingi wa yale ambayo hawakuweza kuyaishi. Hii ndiyo sababu Mungu atawahukumu wanadamu kulingana na habari njema iliyotangazwa na Mtume Paulo, ambayo ndiyo kweli kuu kwamba wokovu haukataliwi kwa mtu yeyote ambaye anamkubali Mungu katika Neno Lake na kumkaribia katika njia Yake.

Je! Njia yake kwa leo ni ipi? “Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka.”

“Kwake yeye asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyemcha Mungu, imani yake inahesabiwa kuwa haki” (Warumi 4:5)

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *