Home 2023 November 25 SABABU YA KUIMBA!

SABABU YA KUIMBA!

SABABU YA KUIMBA!

Wakati wa miaka yao sabini ya utumwa huko Babeli, wana wa Israeli hawakujisikia kuwa ni vyema kuimba:

“Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni? ” (Zaburi 137:1-4)

Tunaambiwa kwamba wana wa Israeli walijulikana sana kwa muziki wao, na wala tusingeweza kushangaa kama hili lingekuwa hivyo, kwa kuwa imani katika Mungu wetu imeongoza nyimbo kubwa na maarufu zisizohesabika katika karne zote. Lakini watekaji wao walipodai kwamba waimbe nyimbo zilizoonyesha shangwe waliyokuwa nayo katika Mungu wao na nchi yao ya asili, huzuni waliyohisi mioyoni mwao haikuwaruhusu mateka hao (wana wa Israeli) kutoa sauti kwa maneno yao huku wakiwa wamefungwa minyororo ya utumwa wa Babiloni.

Lakini je, ikiwa watu wa Mungu hawawezi kuimba nje ya Nchi yao ya Ahadi, Mtume Paulo anawezaje kutuhimiza tuwe “tukisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku tukiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwetu” (Waefeso 5:19)? Tunawezaje kuimba nyimbo za Bwana katika nchi iliyofanywa kuwa ngeni kwetu kwa “hisia” za kumpinga Mungu zinazopatikana pande zote, na uovu juu ya uovu tunaouona kila upande?

Tunaamini ni kwa sababu Mungu wetu tayari “ametufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu” (Waefeso 2:6). Kumbuka, tunamtumikia Mungu “ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako” (Warumi 4:17). Katika kifungu hicho hicho, Mungu aliweza kumwita Abrahamu “baba wa mataifa mengi” kabla hajapata watoto bado. Hii ni kwa sababu Mungu alikuwa ameahidi kuzidisha uzao wake, na hivyo katika mawazo ya Mungu tayari alikuwa na wingi wa uzao! Kwa njia hiyo hiyo, Mungu anatumia wakati uliopita katika kuelezea jinsi ambavyo sisi tayari “tumetukuzwa” (Warumi 8:30), na kwa kuwa Bwana ameahidi kwamba siku moja “tutatawala pamoja Naye” (2 Timotheo 2:2) 12) kutoka kwenye viti vya enzi ambavyo tutaketi pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho, jambo ambalo katika mawazo yake ni kamilifu, na hivyo tuna sifa na uzuri ule tutakaokuwa nao katika siku ya Kristo.

Na ikiwa hicho, sio kitu cha kutufanya tuimbe, hakipo kingine – ASLANI!

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *