Home 2023 November 19 JAWABU LA MUNGU KWA WASIOAMINI!

JAWABU LA MUNGU KWA WASIOAMINI!

JAWABU LA MUNGU KWA WASIOAMINI!

Kufufuka kwa Kristo Yesu ni jibu la Mungu kwa wasioamini na kutokuamini kwao. Mitazamo iliyobadilika ya wafuasi Wake waliomwona akiwa hai baada ya kusulubishwa Kwake na mabadiliko katika maisha ya Mtume Paulo, aliyemtokea “mwisho wa watu wote,” yanashika nafasi ya juu kati ya “dalili nyingi” za ufufuko Wake. Wale waliokuwa waoga walifanywa kuwa wajasiri, wenye shaka waliamini, wenye huzuni walifurahishwa, na yule ‘mtesi’ asiyekuwa na huruma akawa mfuasi wake mwaminifu.

Muhuri wa Kirumi uliovunjwa, kaburi lililokuwa tupu, kushindwa kwa maadui zake Kristo kuleta maiti yake kama uthibitisho wa kutokufufuka kwake na mambo mengine mengi yenye udhihirisho yanaongeza ushuhuda wao katika uthibitisho wa uhakika kwamba Bwana Yesu Kristo “alidhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, …, kwa ufufuo wa wafu” (Warumi 1:4).

Ufufuko wa Kristo Yesu unatuhakikishia kwamba malipo Yake kwa ajili ya dhambi yanatosha na ni kamili, kwa kuwa “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu” (Waebrania 1:3). “Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa” (Waebrania 10:14).

Ndiyo kusema, ufufuo wa Kristo hutupatia Mwokozi aliye hai. Kristo, akilinganishwa na makuhani wa Agano la Kale, Waebrania 7:23-25 ​​inasema:

Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee

Ufufuo wa Kristo pia ni ahadi ya ufufuo wa mwamini katika utukufu. Katika 1 Petro 1:3 Mtume Petro anajitokeza katika usifuji (doksolojia):

“Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu”

Na Bwana wetu Mwenyewe alisema jambo ambalo hakuna mwingine ambaye angeweza kulisema:

“Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi” (Yohana 11:25)

Hatimaye, ufufuo wa Kristo ni onyo kwa ulimwengu juu ya hukumu ijayo:

“Kwa maana [Mungu] ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo hayo, kwa kumfufua [Yesu] katika wafu” (Matendo 17:31)

“Sasa ndio wakati uliokubalika” (2 Wakorintho 6:2)

“Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka” (Matendo 16:31)

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *