Home 2023 October 29 Mtume Paulo Sio Mmoja wa Mitume Kumi na Wawili!

Mtume Paulo Sio Mmoja wa Mitume Kumi na Wawili!

Mtume Paulo Sio Mmoja wa Mitume Kumi na Wawili!

Mara kwa mara, mitume wa Bwana ‘wanashtakiwa’ (wanalaumiwa) kwa kutenda ‘kiholela’ (au kuwa na haraka) katika kumchagua Mathiya kuchukua nafasi ya Yuda. Inasemekana kwanza walichagua wagombea wawili na kisha wakamuuliza Mungu ni yupi kati ya hawa wawili ambaye angelazimika kuchukua nafasi hiyo iliyokuwa wazi. Sauli wa Tarso, ajulikanaye kama Mtume Paulo, kulingana na ndugu hao, ndiye alikuwa chaguo sahihi la Mungu kwa nafasi ya Yuda. Lakini shtaka hilo, halitokani na wala halina msingi wowote wa Kimaandiko. Sababu zifuatazo, ndizo msingi sahihi wa Kimaandiko.

Mitume, pamoja na Petro kama mkuu wao, walikuwa wamepewa mamlaka rasmi ya kutenda katika kutokuwepo kwa Kristo (Mathayo 16:19; 18: 18-20):

“Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.”

“Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”

Walitenda sawasawa kulingana na tangazo la Kimaandiko kwamba mtume mwingine achaguliwe kujaza nafasi ya Yuda (Zaburi109:8; linganisha na Matendo 1:20):

“Siku zake na ziwe chache, Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.”

“Kwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo.”

Kitendo chao ‘kilioshwa’ na siku nyingi za maombi ya pamoja (Matendo 1:12-14), na wagombea wawili walipopatikana waliomba tena na kuacha chaguo la mwisho mikononi mwa Mungu (Matendo 1:24-26):

“Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato. Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.

“Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.”

Yamkini ni wawili tu (Mathiya na Yusufu aitwaye Barsaba) waliostahili, kwa kuwa ni wale tu walioweza kustahili waliomfuata Kristo mfululizo tangu siku ya ubatizo wake na Yohana hadi kupaa kwake mbinguni (Matendo 1:21-22; tazama pia Mathayo 19:28 – “Ninyi mlionifuata mimi”):

“Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu, kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.”

Paulo hangestahiki, kwani hakuwa amemwona Kristo wakati wa huduma Yake duniani (1 Wakorintho 15:8):

“Na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.”

Uthibitisho wa kuhitimisha kwamba wale kumi na mmoja (Thenashara) walitenda kwa mapenzi ya Mungu katika jambo hili unapatikana katika ukweli kwamba Maandiko yanasema wazi kwamba Mathiya “alihesabiwa pamoja na wale mitume kumi na mmoja” (Matendo 1:26) na kwamba “WOTE WALIJAZWA NA ROHO MTAKATIFU” (Matendo 2:4). Wanadamu wanaotenda nje ya mapenzi ya Mungu hawajazwagi na Roho Mtakatifu!

“Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.”

“Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.”

Hivyo Mtume Paulo anasimama kipekee tofauti na wale kumi na wawili kama mtume wa kipindi cha sasa cha neema (Waefeso 3:1-3):

“Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa; ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.”

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *