Home 2023 October 06 ALIHESABIWA PAMOJA NA WAASI!

ALIHESABIWA PAMOJA NA WAASI!

ALIHESABIWA PAMOJA NA WAASI!

“Basi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi” (Marko 15:28)

Utimilifu wa hatua kwa hatua wa kifungu hiki kutoka kwa Isaya 53 ni habari ya kuvutia ya ubatizo mtatu wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwanza, unabii huu lazima utumike kuhusiana na Bwana wetu kupata mwili. Alizaliwa mtoto mchanga huko Bethlehemu, Alibatizwa katika jamii ya wanadamu, akawa, si mmoja tu pamoja nasi, bali pia mmoja wetu, mwanadamu wa kweli, ingawa pia bado alikuwa ni “Mungu halisi.” Hivi ndivyo kwa mara ya kwanza “Alihesabiwa pamoja na wakosaji.”

Baadaye Bwana wetu alibatizwa tena, wakati huu kwa maji, na Yohana Mbatizaji. Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa “toba liletalo ondoleo la dhambi” na wale walioitikia walikuja kwenye ubatizo wake “wakiziungama dhambi zao” (Marko 1:4-5). Si ajabu kwamba Yohana Mbatizaji mwanzoni alikataa kumbatiza huyu asiye na dhambi, akisema: “Mimi nahitaji kubatizwa na Wewe, nawe waja kwangu? Lakini Bwana alisisitiza, akisema: “Ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:13-15). Hivyo Bwana wetu alijiunga na wenye dhambi waliotubu katika ubatizo huo wa Yohana na, kwa njia hii ya vitendo, “Alihesabiwa pamoja na wakosaji.”

Lakini baada ya kubatizwa kwake katika jamii ya wanadamu na ubatizo wake uliofuata wa maji, Bwana wetu alizungumza juu ya ubatizo wake wa tatu, akisema: “Nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe!” (Luka 12:50). Ubatizo huu wa tatu ulikuwa, kwa hakika, kile kifo chake pale Kalvari, ambapo alibatizwa katika hukumu ya Mungu juu ya dhambi ili apate kutuokoa kutoka kwayo.

Hatimaye, basi, Isaya 53:12 ilitimizwa, kwa kuwa ilikuwa ikihusiana na kifo chake pale Kalvari ndipo Marko 15:27-28, inasema:

“Na pamoja naye walisulibisha wanyang’anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. Basi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi.”

Utukufu una Yeye KRISTO Milele na Milele AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *