Home 2023 September 23 UAMSHO MKUU ZAIDI (PAULO II)!

UAMSHO MKUU ZAIDI (PAULO II)!

UAMSHO MKUU ZAIDI (PAULO II)!

Mtume Paulo alipewa huduma mbili tofauti; Huduma yake katika kipindi kinachozungumziwa na Matendo ya Mitume, ilikuwa ni kwa “wasiookoka”. Huduma ya pili ya Paulo baada ya mwisho wa kipindi hicho kinachoshughulikiwa na Matendo ya Mitume, ilikuwa ni kwa “waliookolewa”. Uamsho Mkuu Zaidi ni mwendelezo wa huduma hii ya pili ya Mtume Paulo.

Injili ya awali ya Mtume Paulo ilikuwa ni kwa ajili ya wito na tumaini la ufalme wa kidunia kwa Israeli; Lakini yote hayo yalibadilika mwishoni mwa Matendo ya Mitume. Kazi ya huduma ya pili ilikuwa, na inaendelea kuwa, kwa ajili ya kuwakamilisha (kuwarekebisha) watakatifu (waliookolewa), kwa ajili ya kuujenga (kuuimarisha) Mwili wa Kristo (Waefeso 4:12).

Kwa sababu ya ufunuo huo mpya, Mtume Paulo alipaswa kurekebisha mafundisho yake ya awali na kisha kuhubiri injili hiyo iliyorekebishwa kwa wale ambao alikuwa amewaongoza hapo awali kwenye wokovu. Ilimbidi pia, ajirekebishe kutoka kwenye kuhubiri injili ya ufalme na sasa kuhubiri injili ya Mwili wa Kristo. Hili ndilo lililolazimu kuwepo kwa “seti” yake ya pili ya nyaraka saba.

Mtume Paulo anahitimisha (anajumuisha) huduma yake ya pili katika nyaraka zake kwa watakatifu na waaminifu (waliookoka) huko Efeso na Kolosai kama ifuatavyo:

“Mimi niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo zaidi wa watakatifu wote, nimepewa neema hii ya kuwahubiria mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; na kuwafanya watu wote waone (kuwafunulia watu wote) jinsi ulivyo ushirika wa ile siri, ambayo tangu mwanzo wa ulimwengu ilikuwa imefichwa katika Mungu, aliyeviumba vitu vyote kwa Yesu Kristo” (Waefeso 3:8-9).

“Ambaye sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, na kuyatimiliza katika mwili wangu yale yaliyo nyuma ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa lililoitwa; ambalo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipindi cha Mungu nilichopewa kwa ajili yenu, kulitimiza (kukamilisha) neno la Mungu; Siri hiyo iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi, lakini sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake (waliookolewa) (Wakolosai 1:24-26).

Mtume Paulo alipaswa kuleta nuru kwa yeyote yule, (sawa na katika Yohana 3:16, aliyeookolewa), kipindi cha siri ambacho Mungu alikificha hadi kilipofunuliwa kwake. Siri hii ni kwa wale tu waliookolewa (watakatifu) ambao walichaguliwa na Mungu kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu kuwa viungo vya Mwili wa Kristo (Waefeso 1:4).

“Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; Ambaye hutaka (anatamani) watu wote (sawa na Yohana 3:16 na Waefeso 3:9) waokolewe, na kupata kujua (ujuzi) yaliyo kweli” (1 Timotheo 2:3-4).

Uamsho Mkuu unawapa waliookoka (watakatifu) utangulizi wa ukweli huu mtukufu wa kipindi hiki.

Ndio kusema, ingawa Uamsho Mkuu wa kihistoria wa karne ya 18 ulikuwa na mkazo wake kwa “wasiookolewa” (Yohana 3:16; Warumi 10:9,13); Uamsho huu Mkuu wa sasa una msisitizo wake juu ya “waliookolewa“. Nyaraka za Mtume Paulo kwa Waefeso na Wakolosai zina fundisho la Mwili wa Kristo na fundisho hilo liliandikwa kwa watakatifu na waaminifu: “wale waliookolewa“!

Huduma ya pili ya Mtume Paulo inawaletea “waliookolewa” injili ya Mwili wa Kristo pamoja na wito wake mkuu zaidi. Hii ni nyongeza yenye utukufu kwa injili ya wokovu. ‘Wakristo’ wengi wamepewa ukweli nusu; Unaweza kukubaliana na Malkia wa Sheba aliposhuhudia ufalme wa Sulemani, kwamba “Sikuambiwa nusu”… (1 Wafalme 10:7).

Tambua wewe mwenye, kama ambavyo wengi wamefanya, kwamba kuna mpaka mpya katika mafundisho ya Biblia; hazina iliyofichwa katika Biblia na kwamba “Neno la kweli linashinda mapokeo ya kidini.”

Mtume Paulo aliwaombea watakatifu wote (wale waliookolewa) “ili macho ya mioyo yao yatiwe nuru, wajue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo… wapate kufahamu pamoja na watakatifu wote… na kufanywa upya katika roho ya nia zao. … kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana.

SIFA NA UWEZA NA UKUU VINA YEYE MILELE YOTE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *