Home 2023 September 13 MATENDO 28:28

MATENDO 28:28

MATENDO 28:28

“Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia!”

Huu ni mstari muhimu usioonekana katika kuyagawa Maandiko ambao unaonyesha mabadiliko makubwa ya dhana katika mafundisho ya kimungu. Wokovu wa kitaifa wa Mungu ambao ulikuwa hapo kabla ni pendeleo lenye mipaka la Wayahudi, sasa umeidhinishwa kwa mtu yeyote katika taifa lolote katika ulimwengu huu.

Injili ya Yohana iliidhinishwa kama ujumbe wa uzima wa milele kwa “yeyote” atakayeamini. Paulo alivuviwa kuandika nyaraka mpya saba kuhusu ufunuo mpya kutoka kwa Mungu. Kuna umuhimu mwingine mkubwa wa aya hii (Matendo 28:28) katika kusudi la umilele la Mungu.

Yesu na wanafunzi Wake kumi na wawili walikuwa na injili maalum na hadhira. Wasikilizaji (hadhira) walikuwa ni “kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (Mathayo 10:6, 15:24). Injili yao ilikuwa ni injili ya ufalme kwa Israeli (Mathayo 4:17, 4:23).

Agano Jipya lilipaswa kuwa wokovu na urejesho wa Israeli kupitia Masihi aliyeahidiwa. Lakini ujumbe huo ulikataliwa na Mtume wake akasulubishwa. Hakukuwa na Mmataifa, kama mlengwa, wakati huo; Lengo lilikuwa ni kwa Israeli na tumaini lao la ufalme uliorejeshwa duniani…

Kipindi cha Matendo kilikuwa ni kipindi cha jibu kwa ombi (maombi) ya Yesu akiwa anakufa msalabani. Kipindi cha Matendo kinawakilisha kipindi cha miaka 35 hivi ambapo Wayahudi walipewa nafasi ya kutubu na kutii ujumbe na kumkiri Mjumbe kama Masihi. Mitume walifikiri kihalisi kwamba Kristo angerudi katika kipindi chao ili kurejesha ufalme kwa Israeli. Nyaraka zao zilizoandikwa katika kipindi hiki cha wakati zinawakilisha tumaini hilo na uharaka wa kuwaongoa Israeli ili hili liweze kutokea. Walitiwa nguvu na Roho Mtakatifu kwa karama maalum kama mashahidi kwa Yerusalemu na Uyahudi wote. Wayahudi walipewa hali ya kipaumbele na Mungu…

Hata Sauli (Paulo) aliongoka na kuteuliwa kuwasilisha tumaini hilo kwa Mataifa, wafalme, na wana wa Israeli kwa njia ya Injili ya neema. Kwa takribani miaka 18 tumaini hili la Israeli lilitolewa pia kwa watu fulani wasio Wayahudi ili kuwafanya Waisraeli wawe na wivu. Lakini Wayahudi pia walimkataa Paulo na injili yake ya neema kwa kumfanya akamatwe na kufungwa. Paulo alipofika Rumi; akiwa chini ya kifungo cha nyumbani – mwishoni mwa Matendo ya Mitume, Israeli bado ilishindwa kutubu na kutii. Hii ni mara ya tatu, kwa utawala wa Mungu, kukataliwa na taifa la kibiblia la Israeli.

Taifa la Israeli lilikataa utawala wa Mungu juu yao (1 Samweli 8:7), Yesu Kristo kama mfalme wao na Masihi (Yohana 19:15), na Matendo ya Roho Mtakatifu juu yao (Matendo 28:25).

Kikamilifu, mara tatu, Israeli ilitamkwa kuwa “kipofu, kiziwi, na wajinga” – (Isaya 6:9-10, Mathayo 13:14-15, Matendo 28:26-27)!

Shetani alifikiri kwamba alikuwa amevuruga mpango wa Mungu; lakini Mungu alikuwa na mpango wa siri uliofichwa ambao ungefunuliwa…

Mungu alitoa tangazo la maana sana lenye matokeo mengi katika Matendo 28:28 kupitia maneno ya mtume Paulo:

“Basi ijulikane kwenu, ya kuwa wokovu wa Mungu umetumwa kwa Mataifa, nao watausikia”

KWA KAULI HII:

  1. Mungu aliidhinisha ujumbe wa wokovu kwa watu wote wa mataifa yote BILA kuwa na uhusiano wowote na Israeli.
  2. Mungu alibatilisha hali ya kipaumbele ya Wayahudi iliyokuwa INATAWALA katika kipindi chote cha Injili na Matendo.
  3. Mungu aliita hali ya LO-AMI kwa Israeli kama taifa (Hosea 1:9, 3:4, 6:2).
  4. Mungu ALISIMAMISHA shughuli zake na Israeli katika nyanja zote.
  5. Mungu alinyamazisha REJEA zote kwa maandishi ya Musa na Manabii kama mashahidi.
  6. Mungu ALIONDOA karama za Kiroho (ishara) alizowapa mitume.
  7. Mungu aliahirisha “AGIZO KUU” la Mathayo 28:19-20.
  8. Mungu ALIAHIRISHA kurudi kwa Kristo (iliyotabiriwa na Danieli kutokea katika A.D. 85).
  9. Mungu ALIAHIRISHA kutimizwa kwa Agano la Ibrahimu, la Daudi, na Agano Jipya.
  10. Mungu ALIAHIRISHA kutimizwa kwa unabii wa Danieli wa Majuma Sabini ya Miaka (Na. 8).

Tunajua mambo haya kwa sababu:

  1. Kilichoandikwa na kuachwa kuandikwa katika nyaraka saba za Paulo zilizoandikwa baada ya kipindi cha Matendo kuisha.
  2. Ni nini kilifanyika baada ya kipindi cha Matendo kuisha (k.m. uharibifu wa hekalu mwaka wa 70 A.D.).
  3. Nini hakikutokea baada ya kipindi cha Matendo kuisha (k.m. Kristo hakurudi katika kipindi chao – Mitume).

Matendo 28:28 pia inagawanya:

  • Nyaraka saba za Matendo za Paulo na nyaraka zake saba za baada ya Matendo.
  • Huduma mbili za Paulo: moja katika kipindi cha Matendo ya Mitume na nyingine baada ya kipindi cha Matendo ya Mitume kwisha.

SIFA NA UWEZA NA UKUU VINA YEYE MILELE YOTE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *