Home 2023 September 04 MUSA NA MANABII

MUSA NA MANABII

MUSA NA MANABII

Bwana wetu, alipokuwa hapa duniani, aliwatia watu moyo; Naam na hata kuwapa changamoto wasikilizaji wake “Wayachunguze Maandiko” wao wenyewe (Yohana 5:39). Hakika kwa kuwa Mungu alijifunua Mwenyewe na mpango Wake wa wokovu katika Neno lililoandikwa, tunawajibika, kila mmoja kwa faida yake mwenyewe kujifunza Maandiko.

Yule Tajiri alipomsihi Ibrahimu amruhusu Lazaro kwenda kuwaonya ndugu zake watano juu ya maovu ya kuzimu, Ibrahimu alijibu, “Wanao Musa na manabii; wawasikie wao”. Na yule tajiri alipohimiza kwamba neno moja kutoka kwake lingekuwa na matokeo zaidi, Abrahamu alisisitiza kwamba, “Kama hawawasikilizi Musa na manabii, hawatashawishwa hata kama mtu mmoja atafufuka kutoka kwa wafu” (Luka 16:19-31).

Ndiyo kusema, usimtegemee kasisi wako, mchungaji wako, na wala rafiki yako mpendwa, kukufasiria Maandiko. Jionee mwenyewe kile Mungu anachosema katika Neno lake. Kwa maana “kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu,” inasema Warumi 14:12. Na haitatosha katika siku hiyo kusema kuwa, mhudumu, mchungaji, kiongozi wangu ama kuhani wangu aliniambia hivi na vile! Unawajibika, kibinafsi, kuyachunguza Maandiko wewe mwenyewe, ili kuona kama mambo haya ndivyo yalivyo (Matendo ya Mitume 17:11).

Ni kwa nini huyachunguzi Maandiko, hasa nyaraka za Paulo, mtume wetu watu wa Mataifa? Kwa sababu ni Paulo ndiye asemaye, “Kwa maana nasema nanyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu” (Warumi 11:13). Jifunze katika nyaraka zake fumbo hili kati ya Mataifa ambalo ni Kristo ndani yako tumaini la utukufu na jinsi gani kifo cha Kristo msalabani Kalvari kinaweza kukuokoa. Na ni yeye pia, aliyetuasa tupate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa (1 Wakorintho 4:6).

“Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake” (Waefeso 1:7)

Author: Festus Patta

8 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *