Home 2023 July 07 KWELI YA KRISTO!

KWELI YA KRISTO!

KWELI YA KRISTO!

“Kama vile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu…” (2 Wakorintho 11:10)

Mtume Paulo, mara ngapi, katika barua zake, anazungumza kwa kiapo! “Mungu ni shahidi wangu” (Warumi 1:9), “Kama Mungu alivyo mwaminifu” (2 Wakorintho 1:18), “Angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo” (Wagalatia 1:20), “Mungu ni shahidi wangu” (Wafilipi 1:8), “Nasema kweli katika Kristo, wala sisemi uongo” (1 Timotheo 2:7), n.k.

Kama vile mtu mmoja alivyosema: “Paulo anapotoa taarifa nzito chini ya maana ya uwepo wa Mungu, hakika hasiti kueleza hilo.”

Lakini je, wengine hawakuzungumza chini ya maana ya uwepo wa Mungu? Bila shaka walifanya hivyo, hata hivyo, Mtume Paulo ‘anamwita Mungu atoe ushahidi’ mara nyingi zaidi kuliko mwandikaji mwingine ye yote yule wa Biblia. Ni kwa nini hasa? Jibu linapatikana katika tabia bainifu ya huduma ya Mtume Paulo kama mtume wa ile “siri.”

Yohana Mbatizaji, wainjilisti wanne na wale mitume kumi na wawili hawakuhitaji kusema kwa viapo kwa vile walitangaza yale ambayo tayari yalikuwa yametabiriwa. Lakini kwa Mtume Paulo ilikuwa ni tofauti kabisa. Akiwa ametenganishwa na wale kumi na wawili, ambao walijulikana sana kuwa mitume wa Kristo, Paulo alikuwa ameinuliwa ili kujulisha siri tukufu ambayo Mungu alikuwa ameificha kutoka kwa wote waliokuwa wametangulia. Ingawa mpango huo wa Mungu wa siri hauna mgongano na mpango wa Mungu wa unabii, “siri” hii hata hivyo haikuwa imetabiriwa; ilikuwa ni ufunuo mpya. Kwa hiyo ilikuwa ni jambo lenye ulazima kwa Mtume Paulo kusisitiza tena na tena kwamba aliandika chini ya uwepo wa Mungu.

Hata hivyo, tunapochunguza viapo vya Paulo, ni lazima tujiulize ikiwa kuna yeyote aliyewahi kutumia kiapo hicho kwa unyoofu zaidi. Je, kuna mtu ye yote aliyewahi kuteseka sana kwa ajili ya kweli alizotangaza, au alilipa sana ili kuwasadikisha wengine kuzihusu? Kuna mtu ye yote anayeweza kusema kwa urahisi kama huo kwa wale wanaomjua zaidi?

“Ninyi wenyewe mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote, nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba” (Matendo 20:18-20).

UTUKUFU UNA YEYE KRISTO MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *