Home 2023 June 28 UWEZA MKUU WA MUNGU!

UWEZA MKUU WA MUNGU!

UWEZA MKUU WA MUNGU!

Mnamo mwaka wa 1866 Alfred Nobel aligundua kilipuzi kilichotengenezwa na nitroglycerin. Kilikuwa ni kilipuzi chenye nguvu zaidi ambacho kilikuwa kimevumbuliwa hadi wakati huo.

Nobel na marafiki zake walipoona kile ambacho uvumbuzi wake ungeweza kufanya, ikawabidi waamue juu ya jina; walilitafuta neno lenye kuonyesha nguvu kubwa zaidi – katika lugha zote za ulimwengu. Neno walilochagua hatimaye, lilikuwa ni neno la Kiyunani dunamis!

Neno hili la Kiyunani, lenye kuonyesha nguvu kubwa zaidi, limetumika tena na tena katika Agano Jipya na kwa ujumla limetafsiriwa kama “UWEZA” au “NGUVU”.

Wakati Bwana wetu alipofanya miujiza, kwa mfano, Mwinjili Luka anashuhudia kwamba “UWEZA wa Bwana ulikuwapo apate kuponya” (Luka 5:17). Katika kuwaahidi mitume Wake kwamba wao pia wangefanya miujiza, Alisema: “Mtavikwa UWEZO kutoka juu” (Luka 24:49).

Wakati Masadukayo walipotilia shaka ufufuo, Yesu alijibu: “Mwapotea, kwa kuwa hamyajui Maandiko wala UWEZA Wa Mungu” (Mathayo 22:29), na Mtume Paulo anatutangazia kwamba Kristo “alidhihirishwa kwa UWEZA kuwa ndiye Mwana wa Mungu…” (Warumi 1:4).

Kwa kutumia neno hilo hilo, Mtume Paulo, kwa uvuvio, anatangaza kwamba “Injili ya Kristo ni UWEZA WA MUNGU UULETAO WOKOVU, kwa kila aaminiye…” (Warumi 1:16). Hii ni kwa sababu, kulingana na injili hii, kwamba, “KRISTO ALIKUFA KWA AJILI YA DHAMBI ZETU”, na “KUHUBIRIWA KWA MSALABA”, anasema, kwa waumini ni “NGUVU YA MUNGU” (1 Wakorintho 1:18).

Lakini si tu kwamba waamini wanaokolewa kwa UWEZA wa Mungu; bali pia “WANALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU” (1 Petro 1:5). Kwa hakika, kivumishi cha neno hili hili “dunamis” kinatumika katika Waebrania 7:25, ambapo tunasoma kwamba Bwana wetu Yesu Kristo “AWEZA KUWAOKOA KABISA WAO WAMJIAO MUNGU KWA YEYE…” Hivyo Biblia inatumia neno lenye nguvu sana kwa ajili ya nguvu ili kuonyesha jinsi wokovu wa wale wanaomtumaini Kristo ulivyo salama.

NGUVU NA UWEZA VINA YEYE MILELE YOTE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *