Home 2023 May 28 AHADI MUNGU ALIYOJIWEKEA!

AHADI MUNGU ALIYOJIWEKEA!

AHADI MUNGU ALIYOJIWEKEA!

“Kwa tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu, asiyeweza kusema uongo, aliuahidi kabla ya ulimwengu [au, “zama”] kuanza” (Tito 1:2)

“Wakrete ni waongo siku zote” (Tito 1:12); “Mungu, asiyeweza kusema uwongo” (Tito 1:2) – Tofauti iliyoje! Ni jambo la kutia moyo kwa hakika kujua kwamba wokovu wetu unategemea Neno la Mungu, ambaye hawezi kusema uwongo!

Hata hivyo, kifungu chetu cha utangulizi hapo juu kinasema kwamba Mungu alitoa ahadi hiyo “kabla ya ulimwengu [au, “zama”] kuanza”. Je! Jambo hili linawezekanaje? Hakuna dalili kwamba Mungu aliitoa ahadi hii kwa Malaika, na hakuna mtu mwingine ambaye Mungu angeifanya kwake – isipokuwa kwake Yeye mwenyewe, na huu ndio ukweli kamili wa jambo hilo. Je, sisi nasi hatujajitolea ahadi za dhati kwetu sisi wenyewe?

Kabla Mungu hajatoa ahadi moja kwa mwanadamu yeyote, alijiahidi kwamba angetoa wokovu na utajiri wote wa neema yake kwa wenye dhambi kupitia kazi iliyokamilika ya Kalvari, na ahadi zilizotolewa baadaye kwa wanadamu zilikuwa ni ufunuo wa hatua kwa hatua wa kusudi thabiti alilokuwa nalo tayari katika moyo wake wa upendo. Paulo, mtume wa “siri,” anarejelea tena na tena ukweli huu uliobarikiwa katika nyaraka zake:

“Bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, AMBAYO MUNGU ALIIAZIMU TANGU MILELE, KWA UTUKUFU WETU” (1 Wakorintho 2:7)

“Kama vile ALIVYOTUCHAGUA KATIKA YEYE KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo” (Waefeso 1:4)

“Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, HUKU TUKICHAGULIWA TANGU AWALI SAWASAWA NA KUSUDI LAKE YEYE, AMBAYE HUFANYA MAMBO YOTE KWA SHAURI LA MAPENZI YAKE” (Waefeso 1:11)

“Ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali KWA KADIRI YA MAKUSUDI YAKE YEYE NA NEEMA YAKE. NEEMA HIYO TULIPEWA KATIKA KRISTO YESU TANGU MILELE” (2 Timotheo 1:9)

UTUKUFU NA UWEZA VINA YEYE MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *