Home 2023 May 23 IMANI TUMAINI UPENDO

IMANI TUMAINI UPENDO

IMANI TUMAINI UPENDO

“Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo” (1 Wakorintho 13:13).

Mtume Paulo alikuwa akijadiliana, katika 1 Wakorintho 13, baadhi ya ishara za miujiza ambazo zingetoweka kadiri ufunuo wa Mungu ulivyokamilika. Lakini imani, tumaini na upendo, yeye alitangaza kuwa, vingedumu kama ‘utatu wa uthibitisho’ wa Ukristo wa kweli.

Haya matatu ndiyo yote tunayohitaji katika “wakati huu wa sasa wa neema ya Mungu.” Kanisa lolote ambalo imani, tumaini na upendo hupatikana kwa wingi, hilo ni kanisa “kamili”. Linaweza kuwa na washiriki wachache tu, lakini ni baraka gani kubwa ambayo lingetamani zaidi kuliko imani, tumaini na upendo katika ushirika wake?

Imani, tumaini na upendo ni utatu ambao mara nyingi hurejelewa katika nyaraka za Mtume Paulo. Kila moja ina umuhimu wa msingi kwa njia yake, na hakuna inayoweza kuwepo bila nyingine mbili.

Imani ni ya muhimu sana. Maana Biblia inasema “pasipo imani haiwezekani kumpendeza [Mungu]” (Waebrania 11:6), na Je! Tunawezaje kuwa na tumaini na upendo bila imani?

Tumaini linashikilia nafasi kuu kati ya hizo tatu. Tumaini katika Biblia ni zaidi ya matamanio; ni kinyume cha kukata tamaa, kutazamia kwa hamu baraka zinazokuja. Tumaini ni uzoefu wa Mkristo, kuishi kwake kwa mtazamio wa utukufu wa milele.

Upendo ndio sifa kuu ya wale watatu; ni tunda la imani na tumaini, na ni kubwa zaidi katika maana kwamba ni “kifungo cha ukamilifu.” Zaidi ya hayo, upendo ni wa milele. Siku moja, kwa kila mwamini wa kweli, “imani itatoweka na kuwa dhahiri; tumaini kuwa tupu katika furaha” na upendo utatawala!

Mungu na atusaidie, katika ushirika wetu sisi kwa sisi, ili kuthibitisha kipimo kamili cha imani, tumaini na upendo.

UTUKUFU UNA YEYE MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *