Home 2023 May 21 MAELEKEZO MAZURI!

MAELEKEZO MAZURI!

MAELEKEZO MAZURI!

Mzaha wa zamani ambao ni maarufu sana unasema kwamba sababu iliyowachukua Wayahudi miaka arobaini kufanya safari ya siku kumi na moja kuvuka jangwa (Kumbukumbu 1:2) ilikuwa ni kwa sababu Musa alikuwa ni mtu wa kawaida (sawa na wengine), mkaidi asiyeweza kusimama na kuomba maelekezo!

Bila shaka, wanafunzi wa Biblia wanajua kwamba sababu hasa ya kuchelewa huko ‘kukuu’ kulikuwa ni kwa sababu ya uasi wenye dhambi wa Israeli dhidi ya Mungu. Wakati huo, Bwana aliwaongoza watu wake katika kila hatua ya njia yao kwa wingu (Hesabu 9:15-23); lakini hata hivyo, wingu hilo liliwaongoza katika “kutanga-tanga jangwani miaka arobaini” (Hesabu 32:13) ili kuwaadhibu kwa uasi wao.

Lakini katika kukosekana kwa wingu lolote linalotuongoza leo, tunawezaje kumtarajia Bwana atuelekeze? Je! Mtume Paulo alimaanisha nini hasa alipoandika,

“Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo” (2 Wathesalonike 3:5)

Waumini wengi wa neema wanajua kwamba Mungu huongoza washiriki wa Mwili wa Kristo kwa Neno Lake tu, ingawa bado kunaendelea kuwa na ‘machafuko’ mengi kuhusu hili, kutokana na mistari kama Mithali 16:9:

“Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.”

Mistari kama hii inatumika kufundisha kwamba wanadamu hupanga kile watakachofanya, lakini kisha Mungu anakuja na kuyashinda mapenzi yao na kuwafanya watembee katika njia ambayo ni tofauti na ile waliyopanga. Ufafanuzi huu unatuongoza kwenye namna iliyopindukia ya Ukalvini ambayo inatufundisha kwamba Mungu anawajibika kwa kila hatua wanayofanya wanadamu, kwamba Yeye ndiye Fundi wa kuvuta nyuzi na mwanadamu ni kama mwanasesere anayejibu bila msaada kwa kila matakwa Yake. Mtazamo huu wa Mungu unapakana na kile kinachoitwa ‘jaala’ (fatalism). Watu wengi wasioamini wanaamini kwamba “majaliwa” hudhibiti kila kitu maishani mwetu na hatuna uwezo wa kupindua upungufu wake hata kidogo.

Tatizo la wazi la kuamini kwamba tunaendeshwa na Mwenyezi na hatuwezi kufanya hatua ambayo Yeye haisababishi ni kwamba inamfanya Mungu kuwa ni mwanzilishi wa kila dhambi yetu. Na kwa hiyo ni lazima kuwe na maelezo mengine ya mistari kama Mithali 16:9, na tunaamini kuwa yako. Njia pekee iliyo salama ya kutafsiri Biblia ni kwa kulinganisha Maandiko na Maandiko (1 Wakorintho 2:13), kwa hiyo hebu tulinganishe neno “kuongoza” katika mstari huu na jinsi Isaya alivyotumia neno hilo nyakati zilizopita:

“Ni nani aliyemwongoza roho ya BWANA, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake?” (Isaya 40:13)

Angalia nabii anaposema hakuna anayeweza kumwongoza Roho wa Bwana, anaendelea pia kufafanua maneno yake kwa kusema kwamba Bwana hawezi kushauriwa au kufundishwa. Hivi, ndivyo, Mtume Paulo alimaanisha alipozungumza kuhusu Mungu kuiongoza mioyo yetu. Mungu hutuongoza kwa kutushauri kupitia mafundisho ya Neno lake. Moyo mbovu wa mwanadamu huifikiri njia yake (Yeremia 17:9), na Bwana huja na kumwongoza kufanya kile anachoamuru kwa shauri la Neno Lake.

UTUKUFU NA UWEZA NA UKUU VINA YEYE HATA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *