Home 2023 May 16 UMUHIMU MKUU WA NENO LA MUNGU KWA MUUMINI

UMUHIMU MKUU WA NENO LA MUNGU KWA MUUMINI

UMUHIMU MKUU WA NENO LA MUNGU KWA MUUMINI

Biblia Takatifu siku zote itabaki kuwa na nafasi ya kwanza katika maisha ya Mkristo wa “kiroho”.

Ni jambo la maana sana kuelewe hili, kwa wale wanaojiona kuwa ni wa kiroho zaidi hutoa muda wao mwingi katika maombi; lakini waumini wachache sana, kama wapo, hutoa muda wao katika kujifunza Neno la Mungu. Watu hao, wale wa kundi lile la kwanza, kwa hakika wameangukia kwenye hila danganyifu ya adui ya kucheza na viburi vyao vya asili vya kibinadamu na kuwafanya wajitukuze nafsi zao wenyewe na kumsukuma Mungu nyuma yao.

Kwa kusema hivi, hatupunguzi wala kupuuza hata kidogo umuhimu wa maombi; tunasisitiza tu umuhimu mkuu wa Neno takatifu la Mungu. Katika hili, hakika tupo Kimaandiko kwani Daudi, kwa uvuvio alisema:

“KWA MAANA UMELIKUZA NENO LAKO KULIKO JINA LAKO LOTE” (Zaburi 138:2)

Kwa wale ambao bado wanapinga na kuweka mkazo wa kwanza kwenye maombi badala ya juu ya Neno la Mungu, tunawauliza swali moja rahisi: Je! Ni lipi lililo la maana zaidi, ni lile tulilo nalo la kumwambia Mungu au ni lile ambalo Mungu amelisema kwetu? Kwa hakika kunaweza kuwa na jibu moja tu kwa swali hili, kwa kuwa ni dhahiri kwamba kile Mungu alichosema kwetu ni muhimu zaidi kuliko chochote kile ambacho sisi tunaweza kumwambia. Maombi yetu yamejaa kushindwa kama sisi wenyewe tulivyo, lakini Neno la Mungu haliwezi kushindwa, halibadiliki na ni la milele.

Ilhali wengine, kwa kuwa wameangukia mojawapo ya “hila” za Shetani na kuhisi wako kiroho zaidi juu ya hilo, wako kama mtu mzungumzaji ambaye mtu mwingine humsikiliza na kumsikiliza na kumsikiliza, huku akitingisha-tingisha kichwa kama ishara ya kumkubalia, lakini huku akikosa kabisa fursa ndogo ya “kupenyeza neno.” Wanazungumza mambo mengi bila ukomo, huku wakitoa muda ‘kiduchu’ wa kusikiliza kile ambacho Mungu anawaambia (Waebrania 1:1-2).

UTUKUFU NA UWEZA NA UKUU VINA YEYE HATA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

5 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *