Home 2023 April 16 MATILABA YA SHERIA NA NEEMA

MATILABA YA SHERIA NA NEEMA

MATILABA YA SHERIA NA NEEMA

“Wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti” (1 Timotheo 1:7)

Kwa kuwa “hatuko chini ya sheria, bali tupo chini ya neema” (Warumi 6:15); Je! Mtu anaweza kuwa na nia gani katika kufundisha sheria katika majira haya? Naam, katika siku za Mtume Paulo, watu waliokuwa na uwezekano mkubwa wa kutamani kushikamana na sheria walikuwa ni Wayahudi (Matendo ya Mitume 15:1). Akizungumza juu ya watu hao, Mtume Paulo alimwandikia Tito maneno haya:

“Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.” (Tito 1:10,11)

Jambo ambalo Wayahudi hao waliotahiriwa “hawakupaswa” kuwa wanafundisha ilikuwa ni sheria, ambayo walifundisha kwa sababu ileile ambayo watu wanafundisha sheria hata leo hii – kwa sababu kuna pesa ndani yake. Sikuzote Shetani huhakikisha kwamba ‘ukweli usio na kipimo’ unapendwa na watu wengi, na kufundisha kile kinachopendwa na watu wengi daima ni kazi yenye faida kubwa!

Kwa mfano, katika nyakati zile zilizopita, ujumbe wa Mungu kwa Israeli ulikuwa kwamba angemtumia Nebukadreza kulishinda taifa hilo ili kuliadhibu kwa ajili ya maovu yake (Yeremia 25:9). Lakini manabii wa uwongo katika Israeli walikuwa wakiwahakikishia watu wa Mungu kwamba jambo hilo halingetokea kamwe, na kwamba wao wangeendelea kufurahia amani (Yeremia 23:17). Je! Ni ujumbe gani kati ya hizo mbili unafikiri ulikuwa maarufu zaidi, na hivyo kuleta faida kubwa zaidi?

Bila shaka, Israeli walipokuwa watiifu kwa sheria ya Mungu, ujumbe Wake kwao ulikuwa ujumbe wa amani, lakini walipoasi dhidi ya sheria yake, ujumbe huo ukawa umechelewa kipindi kimoja nyuma. Naam, leo hii sheria imechelewa kipindi kimoja nyuma, lakini ni maarufu na yenye faida kama vile mafundisho ya ‘ukweli usio na kipimo’ yalivyo siku zote. Watu ni ‘wadini’ kwa asili yao, na sheria inavutia “mwili” wao wa kidini (Wagalatia 3:3). Na kile kinachovutia mwili wa kidini wa mwanadamu siku zote kitakuwa biashara maarufu na yenye faida kubwa kama ile inayovutia mwili wake wa kibinadamu (2 Wakorintho 11:20).

Paulo alipoongeza kusema kwamba walimu hao wa sheria walikuwa “hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti,” hiyo ilikuwa ni njia tu yenye adabu ya kusema kwamba ndugu hao hawakujua walichokuwa wakizungumza! Yote haya ni kwa sababu tu walikuwa wamechelewa kipindi kimoja nyuma katika kufundisha yao. Lakini, Je! Hiyo inasema nini kuhusu wale wote “wanaotaka kuwa walimu wa sheria” katika siku zetu hizi za sasa?

Labda inaweza ikawa unafikiri kwamba, “Ikiwa lengo la sheria ni kutufanya tumpende Mungu na jirani zetu (1 Timotheo 1:5), na lakini hatuko chini ya sheria; Je! Hiyo inamaanisha kwamba Mungu hataki sisi tumpende Yeye (Mungu) na majirani zetu pia?” Hakika, Yeye hufanya hivyo! Lakini sasa, upendo huo, ndio lengo la amri mpya. Tambua kwamba, Mtume Paulo aliposema kwamba “mwisho wa amri ni upendo” (1 Timotheo 1:5), hakuwa anarejelea tu lengo la zile amri kumi za Mungu.

Kumbuka, Paulo alifungua waraka wake huo kwa kusisitiza kwamba alikuwa mtume “kwa amri ya Mungu” (1 Timotheo 1:1), na katika maongozi ya neema, lengo la amri hiyo ni upendo kutoka katika moyo safi. Lengo la utume wa Paulo uliowekwa na Mungu ulikuwa ni kuwafanya watu waokolewe na kumpenda Mungu na jirani zao, kama ilivyokuwa chini ya Sheria. Tofauti ni kwamba, katika kipindi hiki, “upendo wa Kristo hutulazimisha” kumtumikia (2 Wakorintho 5:14), sio “hofu” ya kile kitakachotokea kwetu ikiwa tutamwasi, kama ilivyokuwa chini ya sheria. Hiyo ni motisha ya upendo, sio sheria! Hiyo ndiyo motisha ya neema.

UTUKUFU UNA YEYE BWANA MILELE YOTE AMINA

Author: Festus Patta

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *