Home 2023 March 14 FAHARI YETU PEKEE!

FAHARI YETU PEKEE!

FAHARI YETU PEKEE!

“Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo…” (Wagalatia 6:14).

Mtume Paulo wakati fulani alikuwa Farisayo mwenye kiburi, mwenye kujiona kuwa mwadilifu. Katika Wafilipi 3:5-6, anaorodhesha baadhi ya mambo ambayo alijivunia sana:

“Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia.”

Lakini kila kitu kilibadilika tangu siku ile Bwana alipomtokea njiani akiwa anaelekea Dameski. Ghafla alijiona kuwa mwenye dhambi aliyepotea, mwenye hukumu mbele ya Mungu mtakatifu na aliyekuwa ameonja neema isiyo na kifani ambayo imeweza kushuka kutoka mbinguni na kumwokoa hata yeye! Alitambua sasa kwamba hangeweza kusimama peke yake mbele za Mungu mwenye haki, au “kwa miguu yake mwenyewe,” kama tunavyosema. Usalama wake pekee mbele ya ‘kizuizi’ cha Mungu ulikuwa ni kukimbilia na kuwa katika Kristo, kama asemavyo katika Mstari wa 9:

“Tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani.”

Sasa alijua, kama sisi sote tupasavyo kujua, kwamba kimsingi hakuwa na kitu cha kujivunia kuhusiana na msimamo wake mwenyewe mbele za Mungu. Hata hivyo, kwa muda wa maisha yake yote yaliyobakia, alijivunia jambo moja tu: msalaba, ambapo Kristo ambaye yeye (Paulo) alikuwa ‘akimuudhi sana’ alikufa kwa ajili ya dhambi zake ili yeye (Paulo) ahesabiwe haki mbele za Mungu. Mengine yote ambayo Mtume Paulo alijivunia yalikuwa yamekumbatiwa katika msalaba wa Kristo. Hili pia ndilo jambo pekee tunalopaswa kujivunia nalo na kila mtakatifu mcha Mungu zaidi sana ataungana na Mtume Paulo kwa shauku kuu kusema:

“Lakini MUNGU apishie mbali, nisipate KUJITUKUZA, ILA MSALABA WA BWANA WETU YESU KRISTO, AMBAYE KWAKE ULIMWENGU UMESULUBIWA KWANGU, NA MIMI KWA ULIMWENGU.”

Author: Festus Patta

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *