Home 2023 March 10 WIMBO USIOJULIKANA!

WIMBO USIOJULIKANA!

WIMBO USIOJULIKANA!

“Nao walipokwisha KUIMBA, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni” (Mathayo 26:30)

Mara nyingi tumejiuliza (kwa wale wenye muda huo) kwamba ni maneno gani yanaweza kuwa yalikuwa maneno ya wimbo huo mtakatifu, lakini Mungu ameona inafaa kutuzuia tusiyajue kwa sasa.

Katika Biblia zetu tunayo maneno mengi makubwa ya kishairi: Wimbo wa Musa (Kumbukumbu la Torati 32:1-43) – Utukufu mzuri, Zaburi zote na mashairi mengine mengi, lakini wimbo ambao Bwana wetu na Mitume Wake kumi na mmoja waliimba usiku huo kabla ya kuondoka kwenye Chumba cha Juu ulikuwa kwa hakika ni wimbo unaojulikana vyema kati yao, ambao wote waliweza kujumuika pamoja na kuimba. Tunaweza kuwazia na kumwona Bwana wetu akisema, “Kabla hatujaondoka, tuimbe…”!

Hatutajua maneno ya wimbo huo mtakatifu mpaka tufike mbinguni, lakini tunafahamu hili: Bwana wetu na Mitume wake hawakuondoka kwenye kile Chumba cha Juu wakilia na kuomboleza. Ingawa nafsi Yake ilikuwa imefadhaika sana alipokaribia saa ya kutisha ya mateso na kifo Chake, hata aliweza kusema: “Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii” (Yohana 12:27). Ingawa alikuwa amehuzunishwa sana na usaliti wa Yuda, lakini “naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo” (Yohana 13:1), na maneno Yake ya faraja na furaha katika saa hizi za mwisho sasa yamevikwa taji la uimbaji wa wimbo – wimbo, wimbo wa sifa.

Ingawa maneno ya wimbo huo bado hayajajulikana kwetu, somo la uimbaji wake halipaswi kupotea. Kama eneo la Chumba kile cha Juu lilifungwa kwa kuimba wimbo, hakika tunaweza kupewa neema ya kuimba sifa za Mungu katikati ya majaribu yetu haya madogo. Na kama Bwana wetu, Yesu Kristo “ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu” (Waebrania 12:2), hakika mizigo yetu inaweza – na inapaswa – kupunguzwa kwa UJUVI kwamba kwa neema yake, “dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana” (2 Wakorintho 4:17).

UTUKUFU UNA YEYE KRISTO MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *