Home 2023 February 19 ‘IMANI YA KRISTO’ vs ‘IMANI KATIKA KRISTO’

‘IMANI YA KRISTO’ vs ‘IMANI KATIKA KRISTO’

‘IMANI YA KRISTO’ vs ‘IMANI KATIKA KRISTO’

Je! Umewahi kujiuliza kwamba kuna tofauti gani, kama ipo, kati ya ‘imani ya Kristo’ na ‘imani katika Kristo’ inayopatikana katika Wagalatia 2:16 na 3:26? Tafsiri za kisasa zinaonekana kupendekeza kana kwamba misemo hiyo yote miwili ni kitu kimoja.

Wagalatia 2:16

“Hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani YA Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani YA Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.”

dhidi ya

Wagalatia 3:26

“Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani KATIKA Kristo Yesu.”

Roho wa Mungu, kupitia Mtume Paulo, hakukusudia kamwe msisitizo uwe juu ya kile ambacho mwanadamu amekifanikisha, bali kile ambacho Mwokozi amekikamilisha kwa niaba yake. Mtume Paulo, katika vifungu hivyo, anatofautisha wazi misemo hiyo mawili.

Hatuhesabiwi haki kwa kushika sheria, bali tunatangazwa kuwa wenye haki milele kwa imani ya Kristo. Ulikuwa ni uaminifu wa Kristo ambao ndio msingi wa kuhesabiwa kwetu haki. Kwa uaminifu alitekeleza mapenzi ya Mungu Baba ya kutoa ukombozi kwa wanadamu kupitia kazi yake iliyokamilika pale Kalvari (Waebrania 10:5-10).

“Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.”

Ingawa wokovu ni zawadi ya bure inayotolewa kwa wote wanaoweka “imani” yao katika kile ambacho Kristo amefanya, Yeye ambaye ni kusudi la imani yetu, iliyopatikana kwa gharama kubwa. Malipo ya kutukomboa kutoka katika hukumu ya umilele ya dhambi ni damu ya thamani ya Kristo. Ni wale tu, hata hivyo, wanaoiweka imani yao Kwake hao ndio wenye ondoleo la dhambi zao (Waefeso 1:7).

UTUKUFU UNA YEYE MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *