Home 2023 February 16 BWANA ALIPOULIZA ‘KWA NINI?’

BWANA ALIPOULIZA ‘KWA NINI?’

BWANA ALIPOULIZA ‘KWA NINI?’

Kuna nyakati mbili katika Biblia ambapo Bwana wetu, Yesu Kristo aliuliza “KWA NINI?” ambayo ni ya kipekee kuliko ‘kwa nini’ zingine zote!

Mara moja alimlilia Mungu; Mara moja aliuliza kwa Sauli wa Tarso.

Mara moja kwa Mtakatifu sana; Mara moja kwa mkuu wa wenye dhambi.

Mara moja kutoka kwenye msalaba wa aibu; Mara moja kutoka kwenye utukufu wake mbinguni.

Katika kila tukio, jina la mhusika lilirudiwa:

Katika Mathayo 27:46 tunaiona “Kwa nini?” ya kwanza yenye uchungu alipolia:

MUNGU WANGU, MUNGU WANGU, MBONA UMENIACHA?

“Kwa nini?” nyingine inapatikana katika Matendo 9:4, ambapo Aliita kutoka kwenye makao yake mbinguni:

SAULI, SAULI, MBONA WANIUDHI?

Maswali haya mawili yanawakilisha mafumbo makubwa zaidi ya historia, lakini cha ajabu ni kwamba, mojawapo ni suluhu kwa jingine! Kwa nini Mungu alimwacha Mwanawe? Utapata jibu lake utakapouliza kwa nini wanadamu, akiwakilishwa na Sauli, walimwacha na hata kumtesa Mwana wa Mungu! Tendo la Mungu, katika kumtoa Kristo afe, lilikuwa ndilo suluhu kwa mwanadamu. Kifo cha Kristo kilikuwa suluhu – suluhu pekee inayowezekana – kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu. Ilikuwa ni kwa sababu ya ‘kukosa akili kulikopindukia’ kwa dhambi ya mwanadamu ambako Mungu, ili amwokoe wanadamu huyo, ilimpasa atende zaidi ya asivyoweza kueleweka.

Sauli alikuwa ameliongoza taifa lake na ulimwengu katika uasi dhidi ya Kristo, lakini hii ndiyo sababu, Mungu kwa upendo wake usio na kikomo, amchague kuwa mtume mkuu wa neema, akiuambia ulimwengu kwamba “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu.”

Msikie akisimulia jinsi alivyokuwa “mtukanaji, mwenye kuudhi watu na mwenye jeuri” lakini pia jinsi “neema ya Bwana wetu ilivyozidi sana” kwake (1 Timotheo 1:13-14). Msikie akisema:

“Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi. Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.” (Mstari wa 15-16).

Kwa kuwa sasa “mkuu wa watenda dhambi” yuko mbinguni, kuna tumaini thabiti kwetu sote kama tu tutamtumaini Kristo aliyekufa kwa ajili makosa yetu na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.

UTUKUFU UNA YEYE MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *