Home 2023 February 14 SAA MUHIMU ZAIDI YA HISTORIA

SAA MUHIMU ZAIDI YA HISTORIA

SAA MUHIMU ZAIDI YA HISTORIA

Saa muhimu zaidi katika historia yote ilikuwa saa ambayo Bwana wetu Yesu Kristo alikufa msalabani Kalvari kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Mara nyingi, katika Maandiko, saa ya kifo cha Bwana wetu inaitwa kwa urahisi tu “saa,” “Saa yangu,” au “saa yake.”

Ili kutimiza unabii hangeweza kufa saa moja kabla, au moja baadaye: Kabla ya kufika kwa saa hiyo, adui zake walikuwa wamezuiliwa kwa namna fulani wasimdhuru kimwili, hivyo tunasoma katika Yohana 7:30 kwamba:

“Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu SAA YAKE ILIKUWA HAIJAJA BADO” (Angalia pia Yohana 8:20).

Saa hii ilipaswa itimie Kwake wakati wa maumivu yasiyosemeka na aibu isiyoelezeka. Akirejelea hayo, Bwana wetu aliwaambia Andrea na Filipo kuwa,

“Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika SAA HII? Lakini ni KWA AJILI YA HAYO NILIVYOIFIKIA SAA HII” (Yohana 12:27).

Yesu alikuwa amekuja kufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu na sasa hangeweza kuacha mateso yanayohusika. Lakini SAA HII ya mateso na aibu pia ilikuwa ni saa ya utukufu, kwani katika SAA HIYO Mwana wa Mungu alilipa deni ambalo lingezamisha ulimwengu kuzimu. Na hii ndiyo sababu, katika kivuli hicho cha msalaba, Alisema:

“Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi” (Yohana 12:23-24).

“Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele” (Yohana 17:1-2).

UTUKUFU UNA YEYE MILELE NA MILELE AMINA

Author: Festus Patta

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *